Naibu
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta
Nditiye amewataka watanzania kutumia mawasiliano ya simu kwa manufaa ya
kujiletea maendeleo na sio kutumika katika masuala ambayo si sahihi.
Kauli
hiyo wa Naibu Waziri imetolewa jana wakati akifanya uzinduzi wa dua la
simu ambapo ametoa takwimu kwamba asilimia 94 ya watanzania wanatumia
mawasiliano kwa njia ya simu.
Aidha Mh. Nditiye alisema kwamba endapo mawasiliano hayo yatatumiwa vizuri yatasaidia nchi kupiga hatua za kimaendeleo.
Aidha Mh. Nditiye amewataka watoa huduma za mawasiliano kuhakikisha kuna kuwa na huduma bora na zinazokidhi mahitaji.
0 comments:
Chapisha Maoni