Mwanadada
Queen Darlen ameamua kufunguka na kusema kuwa hana ukaribu wowote na
Alikiba zaidi ya kwamba walikuwa wakifanya kazi pamoja na hiyo yote
ilikuwa ni kwa sababu walikuwa chini ya uongozi unaofanana.
Queen Darleen amesema huwa anapoulizwa na media kuhusu Alikiba hapendi kumzungumzia kwa madai kuna watu watatafsiri tofauti.
Wasanii
hao ambao mwanzoni watu walidhani ni ndugu walishafanya wimbo pamoja na
Queen Darleen amesema ni kwasababu kipindi hicho yeye na Alikiba wote
walikuwa chini ya label moja. Queen Darleen amesema Hana ukaribu wowote
na Alikiba tangu zamani ilikuwa ni kazi tu
Pia
akizungumza na GPL Queen Darleen amesema wakati anaanza muziki
takribani miaka 15 iliyopita hakupata usumbufu wa rushwa ya ngono toka
kwa wanaume walio kwenye tasnia Kama baadhi ya wasanii wa kike kwasababu
yeye alishikwa mkono na Dully Skyse kwa hiyo akizinguliwa tu kwa mambo
ya kijinga alikuwa akimwambia Dully .
0 comments:
Chapisha Maoni