Mwenyekiti
wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim
Lipumba amesema anaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano
chini ya Rais Magufuli katika mpango wa ukusanyaji kodi, huku akitaka
utekelezaji huo uzingatie uhalisia
Prof.
Lipumba ametoa kauli hiyo leo wakati alivyokuwa anazungumza na
waandishi wa habari baada ya ukimya wake wa muda mrefu na kusema Baraza
kuu la Chama cha Wananchi CUF linaitaka mamlaka inayohusika na masuala
ya ukusaji wa kodi kwa wafanyabiashara wawe wanatoa makadirio mazuri ili
kuweza kuwapa fursa wateja zao kulipa kodi vizuri.
"Baadhi ya makampuni na wafanyabiashara wanakadiriwa kodi kubwa kuliko wanachouza na hatimaye biashara zao zinafungwa.
"Baraza
kuu la Chama cha Wananchi CUF linaitika serikali ifanye makadirio ya
kodi ambayo yatakuwa yanazingatia hali halisi, Mamlaka ya kodi
isiwakamue wafanyabiashara mpaka biashara kufungwa na kusababisha kupata
hasara", amesema Prof. Lipumba.
Pamoja na hayo, Prof. Ibrahim Lipumba ameendelea kwa kusema "tunaunga
mkono katika ukusanyaji wa kodi lakini utekelezaji wake uzingatie hali
halisi, tusije tukawakamua watu wanaofanya biashara, wenye makampuni
ambao wanatoa ajira mpaka biashara na shughuli zao kupelekea kuzifunga".
Kwa
upande mwingine, Prof. Lipumba amedai Baraza kuu limepata kuwepo kwa
malalamiko ya hali ya maisha kuwa magumu kupitiliza na kuiomba serikali
iongeze mzunguko wa pesa ili kuweza kuinua maisha ya watanzania wa hali
ya chini.
0 comments:
Chapisha Maoni