Shughuli
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zilisimama kwa muda baada ya
kutokea kwa hitilafu ya umeme katika transfoma ya Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco) iliyopo katika eneo la mahakama hiyo.
Trasfoma
hiyo imelipuka na kusababisha nyaya mbili kushika moto na kuzua hofu
miongoni mwa watu waliokuwa mahakamani hapo, kuanza kukimbia hovyo.
Tukio hilo limetokea leo asubuhi Machi 1, 2018 wakati kesi mbalimbali zikiendelea kusikilizwa.
Mtendaji
wa Mahakama Mkoa wa Dar es Salaam, Gasto Kanyairita amesema baada ya
kutokea kwa mlipuko huo ulizuka moto na kushika nyaya mbili, ikiwemo ya
intaneti ambazo hutumiwa kwa ajili ya mawasiliano ya simu.
"Moto uliingia moja kwa moja katika jengo letu na kushika seva yetu ambayo tunatumia kwa ajili ya mawasiliano ya simu,” amesema.
"Baada
ya kushika nyaya hizo, moto huo uliambaa amba na kuingia katika chumba
cha Tehama na kisha kushika soketi ya umeme iliyopo ndani ya jengo la
mahakama.”
Baada
ya kutokea kwa hitilafu hiyo ya umeme, askari polisi walikuwepo
mahakamani hapo, alitumia vidhibiti moto na kufanikiwa kuuzima.
Dakika tano, baada ya kutokea kwa hitilafu hiyo, gari la zimamoto lilifika mahakamani hapo na kukuta tayari moto huo umezimwa.
0 comments:
Chapisha Maoni