WAZIRI
wa Fedha na Mipango,Dk. Philip Mpango amepiga marufuku kwa shirika
lolote kufanya makadirio ya idadi ya watu wa Tanzania na kuchapisha
matokeo hayo bila kushirikisha Ofisi ya Taifa ya Takwimu na
atakayebainika kufanya hivyo watamchukulia hatua kali za kisheria.
Dk.Mpango
amesema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati anazindua taarifa ya
makisio ya idadi ya watu Tanzania ambapo alisema kwa makadirio
yaliyotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
Viwango vya uzazi na vifo kwa takwimu za mwaka 2016, idadi ya watu Tanzania sasa ni milioni 54.2 ambapo Tanzania Bara ni watu milioni 52.6 na Tanzania Bara watu milioni 1.6 kwa mwaka 2018.
Dk.Mpango aliisema idadi hiyo inakadiriwa kufikia watu milioni 59.4 mwaka 2021 na ifikapo mwaka 2030 idadi ya watu itafikia milioni 77.5.
Pia
Dk.Mpango aliwakumbusha wadau wote wa ndani na nje ya nchi kuwa takwimu
za idadi ya watu kwa nchi ya Tanzania ni hizo ambazo amezitangaza jana
na si vinginevyo.
Alifafanua
kwa kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012
inakadiriwa kuwa kila mwaka kuna ongezeko la wastani watu wapatao
milioni 1.6 hapa nchini.
Dk.Mpango
alisema ongezeko hill linatokana na idadi kubwa vya vizazi vipatavyo
milioni 2.0 ikilinganishwa na idadi ndogo ya vifo ambavyo ni takribani
400,000 kwa mwaka.
“Utafiti
wa mama na mtoto wa mwaka 2015/16 unaonesha kwamba mwanamke wa
kitanzania atazaa watoto watano katika maisha yake yote ya uzazi .
”
Hata hivyo kiwango cha uzazi kilipungua kutoka wastani wa watoto 7
mwaka 1978 had I wastani wa watoto watano mwaka 2016.Baadhi ya sababu za
juu cha uzazi ni kiwango kikubwa cha vifo vya watoto,familia kupendelea
kuwa na watoto wengi,umasikini,mila,imani za kidini na matumizi madogo
ya uzazi wa Mpango,”alisema.
Aliongeza
matokeo yake ni kuwa na idadi ya watu hapa nchini imeendelea kuongezeka
na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya sita katika Bara la Afrika kwa kuwa
na idadi kubwa ya watu baada ya Nigeria, Ethiopia, DRC na Misri.
Alisema
kwa mtazamo wake wingi au au uchache wa idadi ya watu sio tatizo bali
tatizo ni pale ambapo kasi ya ongezeko la idadi hiyo inazidi kasi ya
ukuaji wa uchumi na hivyo kulifanya Taifa kushindwa kumudu ipasavyo
mahitaji ya wananchi.
Dk.Mpango
alisema kasi ya ongezeko la idadi ya watu pia inaleta changamoto ya
idadi kubwa ya watoto na vijana .”Kwa mfano takwimu nilizozizindua leo
zinaonesha asilimia 50 ya watu wote nchini ni watoto wenye umri chini ya
miaka 18.
“Asilimia
hii kubwa ya watoto katika nchi zinazoendelea inatokana na mabadiliko
ya kidemografia kutoka viwango vya juu vya vifo lakini wakati huo
viwango vya uzazi vibaki juu,” alisema.
Aliongeza
asilimia kubwa ya watoto ni changamoto kwa maendeleo ya nchi yoyote
duniani kwa vile kundi hilo lina mahitaji ya kipekee ambayo lazima
yatimizwe na Serikali na jamii kwa ujumla wake.
Dk.Mpango alisema mojawapo ya changamoto hizo ni kiwango cha juu cha utegemezi kinachotokana na idadi kubwa ya watoto.
Alisema
kwa mfano kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kiwango
cha utegemezi kiumri ni asilimia 92 ikilinganishwa na wastani wa
asilimia 40 kwa nchi zinazoendelea.
Hiyo
ikiwa na maana kuwa kwa Tanzania kila watu 100 wenye umri wa miaka 15
hadi 64 wanategemewa na watu 92 wenye umri chini ya miaka 15 wenye umri
zaidi ya miaka 65.
0 comments:
Chapisha Maoni