Kesi
ya kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili
mbunge wa Kawe, Halima Mdee leo March 29, 2018 imeshindwa kuendelea
baada ya mshtakiwa kuwa mgonjwa.
Kesi
hiyo imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
kutokana na mshtakiwa huyo kuwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu.
Mdee
anakabiliwa na shtaka moja la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais, kwa
kusema, “anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afungwe breki” kitendo ambacho
kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Wakili
wa Serikali, Patrick Mwita amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Thomas Simba wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kuendelea na
ushahidi.
“Kesi
hii imekuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi na tayari upande wa
mashtaka tunaye shahidi hapa mahakamani, lakini nimepata taarifa kuwa
mshtakiwa ni magonjwa na ameshindwa kufika mahakamani hapa,” -Wakili
Mwita.
Baada
ya kueleza hayo, wadhamini wa Mdee, Fares Robison ambaye ni Diwani wa
Mbezi Juu na Martha Mtiko Diwani wa viti maalumu, wameieleza mahakama
hiyo kuwa Mdee yupo Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu. Baada ya
maelezo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi May 3, 2018
itakapoendelea na ushahidi.
0 comments:
Chapisha Maoni