Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na Naibu
wake, Juliana Shonza, leo wametangaza kufuta adhabu ya kufungia wasanii
wa muziki wa Kizazi Kipya, Roma Mkatoliki na Suzan Michael maarufu kama
Pretykind.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam
Waziri Mwakyembe amesema kuwa muda wowote kuanzia sasa Roma Mkatoliki
atakuwa huru kufanya shughuli zake za muziki kama ilivyokuwa awali kwa
sharti moja la kukamilisha taratibu za kujisajili BASATA.
Kwa
upande mwingine, Roma Mkatoliki ambaye naye aliongozana na Waziri
Mwakyembe amesema kuwa hata kama ameachiwa huru lakini wimbo wake wa
kibamia ataviomba vituo vya redio na runinga kutocheza wimbo huo.
Mwanzoni
mwa mwezi Machi serikali kupitia Wizara ya Habari ilitangaza kumfungia
miezi sita msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na masuala ya muziki kwa
kukaidi amri ya kubadilisha baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa Kiba100.
Suzan Michael maarufu kama Pretykind naye alipewa nafasi ya kuongea na wanahabari ambapo alitoa pongezi kwa serikali kwa kumfundisha malezi mema na kuwaasa wasanii wenzake kuwa na tabia nzuri.
Suzan Michael maarufu kama Pretykind naye alipewa nafasi ya kuongea na wanahabari ambapo alitoa pongezi kwa serikali kwa kumfundisha malezi mema na kuwaasa wasanii wenzake kuwa na tabia nzuri.
0 comments:
Chapisha Maoni