Mdhibiti
na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Profesa. Mussa Assad ameomba
radhi wananchi na serikali juu ya taarifa ya deni la taifa na kusema
kuwa yalifanyika makosa ya kimatamshi, deni hilo ni himilivu.
Profesa
Assad ametoa taarifa hiyo mjini Dodoma ambapo amesema deni halisi ni
shilingi trillion 46.08 na ni himilivu hivyo anaomba radhi kwa usumbufu
uliojitokeza kwa wananchi na taasisi za serikali.
CAG
wakati akitoa ripoti hiyo kwa Rais John Pombe Magufuli kuhusu suala la
muenendo wa deni la taifa alidai kuwa deni la taifa si himilivu lakini
kwa mujibu wa utafiti ambao wamefanya wao CAG ameibuka na kuomba radhi
na kusisitiza kuwa ripoti ya CAG ni siri hadi itakapowasilishwa
bungeni.
0 comments:
Chapisha Maoni