Msanii
wa filamu nchini Kajala Masanja amefunguka na kuweka wazi kuhusu tetesi
zinazosambaa kuwa sasa anatoka kimapenzi na msanii wa muziki wa Bongo
fleva kutoka kiumeni Chege Chigunda.
Kajala
akiomgea kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio amekana
kuhusu kutoka kimapenzi na msanii huyo na kudai kuwa hakuna jambo kama
hilo na
"Mama
yangu mzazi hakuna kitu kama hicho si mmeona Chege kapata mtoto juzi tu
hapa, yaani mimi sina hata namba yake ya simu na haiwezi kutokea kitu
kama hicho"alisisitiza Kajala
Mbali
na hilo Kajala amewatakia kheri wanawake wote maarufu ambao wanakaribia
kuolewa siku za karibuni na kusema kwake yeye badobado kwani anaamini
mume mwema anatoka kwa Mungu hivyo atakapompata huenda na yeye ndiyo
akafanya maamuzi hayo ya kuolewa sasa.
0 comments:
Chapisha Maoni