JESHI
la Polisi mkoani Pwani limewaasa madereva hususani wa mabasi
yanayofanya safari za mikoani ,kuacha kufanya mbwembwe wakati wakiwa
barabarani na kutumia vileo katika kipindi hiki cha sikukuu za Pasaka
ili kuepusha ajali zembe.
Aidha jeshi hilo limetoa onyo kali kwa wale wenye nia ya kutenda uhalifu kwenye kipindi hicho .
Akizungumza
na waandishi wa habari na baadhi ya maofisa wa jeshi hilo ,kuhusiana na
operesheni za kaguzi hizo ambazo ni endelevu ,na kutoa salamu za Pasaka
,kaimu kamanda wa polisi ,mkoani Pwani ,(SSP) Abdi Issango ,alisema
madereva wafuate sheria za usalama barabarani bila kushurutishwa .
Amesema
wanafanya operesheni ya kukagua madereva wa mabasi hayo na kufanikiwa
kuwakamata madereva 29 kwa makosa ya mwendo kasi na kulipita gari la
mbele sehemu isiyoruhusiwa (wrong overtaking).
Pamoja na hayo ,Issango alielezea madereva 22 walikamatwa kwa kosa hilo na madereva saba walikamatwa kwa kosa la mwendo kasi .
Alibainisha
dereva mmoja alipewa onyo kutokana na kosa lake ,madereva watano
waliadhibiwa kwa kulipishwa faini ,na madereva 23 watafikishwa
mahakamani kuweza kujibu mashtaka yanayowakabili .
"Katika
operesheni hii ,dereva wa kampuni ya basi la Super Feo lenye namba za
usajili T.754 DML linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam -Songea
,Peter Augustino (38) mkazi wa Makambako "
"
Yeye tutamfikisha mahakamani kwa makosa mawili ya kulipita gari la
mbele sehemu isiyoruhusiwa na kuendesha gari akiwa ametumia kileo
ambapo baada ya kumpima alikutwa akiwa na kilevi 26.8mg/ml.":;alisema
Issango.
Kwa
mujibu wa Issango machi 28 mwaka huu jeshi hilo limeendesha msako
katika maeneo mbalimbali katika mkoa huo na kufanikiwa kukamamata
watuhumiwa 21 wakiwa na bangi kete 155 sawa na gramu 77.5.
Alisema
huko Mapinga wilayani Bagamoyo ,walimkamata Wilson Jengua akiwa na
mtambo mmoja wa kutengeneza pombe ya moshi(gongo) , "Mbali ya mtambo huo
,tumekamata pombe hiyo lita 62 " alifafanua Issango.
Issango
ambae pia ni kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Pwani,
alieleza watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yao .
Aliwasihi
wahalifu wenye mawazo ya kufanya uhalifu kipindi cha Pasaka wabadili
mawazo hayo, kabla ya hatari kwani jeshi hilo limejipanga kikamilifu
kupambana na uhalifu wa aina yoyote.
0 comments:
Chapisha Maoni