Urusi
imewafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani, na kufunga ubalozi uliopo St
Petersburg ikiwa ni majibu kwa kitendo cha Marekani kuwafukuza
wanadiplomasia wa Urusi juu ya shutuma ya Uingereza kuhusu kuhusika kwa
Urusi katika shambulio la jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Kripal na
binti yake huko Uingereza.
Hatua
hiyo ilitangazwa na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov.
Zaidi ya nchi ishirini zimewafukuza wanadiplomasia wa urusi nchini mwao
katika kuunga mkono Uingereza.
Miongoni mwa nchi hizo ni Marekani ambapo mapema wiki hii iliwatimua wanadiplomasia 60 wa urusi kuondoka Marekani.
Katika
kujibu hilo Urusi imewatimua wanadiplomasia 58 kutoka Moscow na wawili
kutoka mji wa Yekaterinburg, chombo cha habari cha Interfax kiliripoti.
Lavrov alisema kuwa nchi nyingine zilizowafukuza Warusi wasubiri majibu kwa vitendo.
Ameongeza
kuwa Ubalozi wa Marekani umepewa taarifa juu ya hatua hiyo kama majibu
kwa Marekani kwa kuwatimua wanadiplomasia wake na kusimamisha ubalozi
ulioko St. Petersburg.
Baada
ya hatua hiyo msemaji wa Marekani amesema kuwa Urusi haina nia ya kuwa
na uhusiano mzuri na nchi nyingine, na hivyo Marekani ina haki ya
kuchukua hatua nyingine dhidi ya Urusi.
''Urusi imeamua kujitenga zaidi yenyewe, tunaangalia maamuzi ya kuchukua'' Heather Nauert aliwaambia waandishi wa habari.
Urusi
imekataa kuhusika kwa namna yoyote na jaribio la mauaji kwa jasusi wake
wa zamani. Kripal bado yupo katika hali mbaya hospitalini lakini Binti
yake anaendela vizuri na ameondoka katika hali ya hatari.
Kutokana
na kuhusishwa kwa Urusi na tukio hilo mapema Uingereza ilisema kuwa
hawatatuma mawaziri wake pamoja na familia ya Malkia kushiriki kombe la
dunia.
Itakumbukwa kuwa mwaka 1986 Rais wa Marekani Ronald Reagan aliwatimua wanadiplomasia 80 wa Urusi.
Na mwaka 2016 uongozi wa Barack Obama uliwafukuza wanadiplomasia 35 kutokana na kudukua chama cha Democratic.
Credit:BBC
Credit:BBC
0 comments:
Chapisha Maoni