Mahakam
nchini Kenya imewapiga faini waziri wa mambo wa mambo ya ndani Fred
Matiang'i na mkuu wa jeshi la polisi Joseph Boinnet baada ya wawili hao
kudharau amri yake kuhusu kumuachia mwanasiasa wa upinzani Miguna Miguna
Waziri
wa mambo ya ndani wa Kenya na Inspekta Janerali Mkuu wa Polisi
wamepigwa faini kwa kuidharau mahakam siku ya Alhamisi, kwa kushindwa
kutii agizo la jaji kumuachia mwanasiasa wa upinzani, katika hukumu
iliochochea zaidi mgogoro kati ya mihimili miwili ya dola.
Jaji
wa mahakama Kuu George Odunga amesema maafisa hao wawili waandamizi
serikalini "walidhihirsha tabia isiyotarajiwa katika zama hizi za
kikatiba," - katika ukaripiaji usiokifani kwa maafisa wa juu serikalini.
Waziri
wa mambo ya ndani Fred Matiang'i, na inspekta Jenerali Mkuu wa Polisi
Joseph Boinet wametozwa kila mmoja shilingi za Kenya 200,000, sawa na
dola za Marekani 1,985, kutokana na ushiriki wao katika kumzuwia
mwansiasa wa upinzani Miguna Miguna wiki hii.
Mahakama
nchini Kenya imekuwa katika msuguano na mhimili wa utawala tangu
ilipobatilisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa Agosti
2017.
Miguna
Miguna, mwanasiasa maarufu lakini asiechaguliwa kutoka muungano wa
upinzani wa NASA, alijipatia umaarufu baada ya kufukuzwa nchini mwezi
uliopita, na jaribio lake la kurejea Kenya wiki hii limeshuhudia nchi
hiyo ikiingia katika sarakasi za kisiasa.
Wakati
Miguna alipozuwiwa kwenye uwanja wa ndege kuhusiana na mgogoro wa
uhamiaji, mahakama kuu iliwaamuru mara mbili, waziri wa mambo ya ndani
Fred Matiang'i, mkuu wa jeshi la polisi Joseph Boinnet na kamishna mkuu
wa idara ya uhamiaji kumfikisha mahakamani.
Mvutano kati ya mihimili mikuu miwili
Vita
vinavyozidi kati ya serikali na mahakama - tangu mahakama ya juu
kabisaa ilipobatilisha ushindi wa rais Uhuru Kenyatta mwaka uliopita --
vimeshuhudia maafisa wa serikali wakipuuza amri kadhaa za mahakama.
Kufukuzwa
kwa kwanza kwa Miguna kulikuja baada ya kukamatwa kwa tuhuma za uhaini
kutokana na kushiriki kwake katika tukio la kujiapisha kwa Raila Odinga,
aliesisitza kuwa yeye ndiye alikuwa mshindi halali wa uchaguzi wa mwaka
uliopita.
Wizara
ya mambo ya ndani ya Kenya inasema Miguna alipoteza uraia wake kwa
kuchukuwa uraia wa Canada miaka kadhaa iliopita -- wakati ambapo uraia
wa nchi mbili ulikuwa hauruhusiwi.
Mwezi
Februari, mahakama iliiamuru serikali kumruhusu Miguna arejee, na
kumpatia hati mpya ya kusafiria au imruhusu aingie nchini kwa kutumia
hati yake ya Canada, wakati akisubiri kusikisiliza shauri la kutetea
uraia wake wa Kenya.
Hata
hivyo, Miguna alipowasili siku ya Jumatatu, alikataa kuomba visa ya
miezi sita, kuingia kwa kutumia hati yake ya Canada au kujaza fomu za
kuhalalisha uraia wake.
"Alikataa
kusaini nyaraka za kuingia nchini na kuzichana. Alisalia hapa kwa siku
mbili na kila zilipopelekwa kwake alitukaripia kwamba yeye ni Mkenya,"
alisema afisa uhamiaji kwa sharti la kutotajwa jina.
Polisi wamalizia hasira kwa waandishi
Siku
ya Jumatatu, polisi wa uwanja wa ndege waliwashambulia na kuwajeruhi
waandishi kadhaa wa habari waliokuwa wanaripoti sakata hilo katika tukio
lililorekodiwa na kulaaniwa na kamati ya kuwalinda waandishi habari.
Katika
taarifa kutoka Dubai, Miguna alisema alizuwiwa chooni kwa siku mbili
katika uwanja mkuu wa ndege wa Kenya, na kudai kuwa maafisa
walimuangusha chini na kumpiga sindano yenye vitu visivyoeleweka na
kumsababishia kupoteza fahamu.
0 comments:
Chapisha Maoni