Mahakama
ya Hakimu ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewapatia dhamana viongozi sita wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), bila washtakiwa hao kuwapo
mahakamani huku wakitakiwa kuripoti kila Alhamisi.
Awali,
viongozi hao akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe,
walidhaniwa kuletwa mahakamani hapo na mahakama ikaamua kuketi na
mawakili wa pande zote mbili kujadili kama washtakiwa hao wataletwa au
la ili itoe uamuzi wake.
Baada
ya makubalianao hayo, Inspekta Shabani wa Magereza ameieleza mahakama
kuwa washtakiwa hao wameshindwa kuletwa mahakamani hapo kwa sababu gari
la kuwaleta ni bovu.
Akitoa
uamuzi wake, Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri amewataka washtakiwa hao
kuwa na wadhamini wawili kila mmoja na kusaini kwa maandishi ya Sh
milioni 20.
“Kila
mshtakiwa atasaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 20, wadhamini pia
watasaini kiwango hicho, washtakiwa wakiwa nje kwa dhamana wanatakiwa
kuripoti polisi mara moja kwa wiki, ambayo ni kila siku ya Alhamisi,” amesema.
Baada
ya maamuzi hayo,Wakili wa serikali, Faraja Nchimbi ameieleza Mahakama
kuwa wataka rufaa kupinga uamuzi wa mahakama hiyo kutoa masharti ya
dhamana kwa Mbowe na wenzake.
Pamoja
na Mbowe, viongozi wengine ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent
Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa
na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ambao wanakabiliwa na mashtaka
manane yakiwamo kuhamasisha maandamano, uchochezi na uasi.
0 comments:
Chapisha Maoni