Mtoto
Mase Denis kutoka Kabwana wilayani Rorya mkoani Mara aliyedaiwa
kunajisiwa na baba yake wa kufikia Machi 3, mwaka huu alifariki dunia
wakati akiwa njiani kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Rufani Bugando
jijini Mwanza juzi.
Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime-Rorya, Henry Mwaibambe aliwaambia
waandishi wa habari kuwa awali mtuhumiwa Denis Ondigo alishitakiwa kwa
kunajisi lakini kutokana na kifo hicho amebadilishiwa kuwa shtaka la
mauaji.
Mtuhumiwa
anadaiwa kutenda kosa hilo majira ya saa 6 mchana wa Machi 3 akiwa
nyumbani kwake Kabwana baada ya mama wa mtoto kuwa amekwenda dukani
kununua mahitaji ya nyumbani.
Kamanda
huyo alisema Ondigo (26) mkazi wa Kabwana alifikishwa Mahakama ya
Wilaya Tarime mkoani Mara kwa mara ya kwanza Machi 13.
0 comments:
Chapisha Maoni