test

Jumamosi, 17 Februari 2018

Taarifa Kuhusu Mwanafunzi aliyepigwa Risasi na Polisi


Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) imepokea kwa mshituko taarifa za kifo cha mwanafunzi Aqulina Akwilini ambaye inasemekana amepigwa risasi na polisi wakati wakikabiliana na waandamanaji wa Chadema jana.

Awali taarifa hizo zilimhusisha mwanafunzi huyo na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) lakini baada ya uchunguzi wa kina imebainika ni mwanafunzi anayesoma Chuo cha Usafirishaji (NIT) mwaka wa kwanza.

Daruso inalaani vikali kitendo hicho kilichotokea na kutumia nafasi hii kushauri polisi kujitafakari kama ni sahihi kupambana na raia wa Tanzania kwa kutumia silaha za moto.

Daruso pia amekitaja kitendo hicho kuwa ni cha kinyama na cha kulaaniwa na kukemewa na kila Mtanzania yeyote bila kujali tofauti  za kisiasa.

‘’Pamoja na tofauti zetu nyingi kama vyama , dini ,ukabila na kadhalika , taifa letu limejengwa kwenye misingi ya undugu, umoja, mshikamano na si matumizi ya nguvu kupita kiasi au kukiuka sheria na taratibu za nchi yetu,’’ imesema barua hiyo ya Daruso kwa vyombo vya habari.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni