Wafuasi
hao wa CHADEMA wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe
waliandamana kuelekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni,
Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa uchaguziwa chama hicho.
Maandamano
hayo yalianzia viwanja vya Buibui Mwananyamala ulikokuwa ukifanyika
mkutano wa kampeni wa Chadema na yalipofika eneo la Mkwajuni wafuasi hao
walitawanywa na polisi, huku mtu mmoja aliyekuwa kwenye basi la
daladala akidaiwa kupigwa risasi na kufariki dunia
Kamanda
Mambosasa amesema kuwa watu hao waliokuwa wakiandamana, walizuia mabasi
yanayotoa huduma ya usafiri wa mwendokasi, na kuanza fujo kwa kurusha
mawe, hivyo polisi waliingilia kati na kuwatawanya kwa kufyatua risasi
kadhaa hewani, na kati ya risasi zilizofyatuliwa, moja ilimpata mtu.
“Walizuia
mwendo kasi, wakaanza kupiga mawe kwa hiyo kati ya risasi za hewani
zilizopigwa kuwatawanya kuna iliyompata (mtu),” alisema.
Ufafanuzi
huo wa Mambosasa licha ya kutoweka wazi kama mtu huyo aliyepatwa na
risasi hiyo amefariki dunia ama la, umekuja huku ikidaiwa kuwa
aliyepigwa risasi na kupoteza maisha ni mwanafunzi wa elimu ya juu.
Taarifa
za kifo cha mwanafunzi huyo zilianza kusambaa tangu jana, Ijumaa jioni
katika mitandao ya kijamii sambamba na kuwekwa picha yake huku ikieleza
kuwa amepigwa risasi wakati akiteremka katika basi la daladala.
Mambosasa
alipoulizwa kama mtu huyo ni mwanafunzi wa elimu ya juu amesema kuwa
haijathibitishwa kama ni mwanafunzi nab ado uchunguzi unaendelea ili
kubaini ukweli wa jambo hilo.
“Haijathibitishwa hiyo, nipo kwenye pilika za uchaguzi, nadhani nitajibu hilo nitakaporejea ofisini na kupata taarifa,” alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni