test

Jumamosi, 17 Februari 2018

Mgombea Ubunge wa CHADEMA Kinondoni Salum Mwalimu Akamatwa na Polisi


Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu amekamatwa  na polisi katika kituo cha kupigia kura cha Idrisa kata ya Magomeni.

Tukio hilo limetokea Muda mfupi baada ya  baadhi ya wananchi wa kata hiyo kudai kuwa katika kituo hicho kuna mtu ametoroka na sanduku lenye kura, baadaye kukamatwa na polisi akiwa amelibeba sanduku hilo.

Mwalimu  aliyefika kufatilia undani wa tukiio hilo la kuibiwa Sanduku, alikamatwa nje ya kituo hicho na kupakizwa katika gari la polisi aina ya defender huku taarifa za awali zikidai kuwa alikwenda eneo hilo na kundi kubwa la watu.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwa Mwalimu amesema kuwa hana taarifa zozote.

Baada ya kufikishwa kituo cha polisi Magomeni, Mwalimu aliingizwa ndani na kukaa takribani robo saa na kuachiwa

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni