Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Kinondoni (CHADEMA) Salum Mwalimu amedai sanduku la
kupigia kura katika mtaa wa Idrisa Magomeni Jijini Dar es Salaam
limeibwa huku watu wakishuhudia kitendo hicho kikifanyika na hakuna
hatua zozote za kisheria zilizofanyika
Salum
Mwalimu amebainisha hayo pindi alipokuwa anazungumza mubashara kutoka
katika kituo hicho baada ya kupata taarifa kutoka kwa mmoja wa wakala
wake aliyempigia simu kumtaarifu kwamba kuna mtu ameiba sanduku la
kupigia kura akiwa na gari na kutokomea pasipo julikana.
"Nimepigiwa
simu na wakala wangu kuwa sanduku lilikuja na kuibwa lakini
nikazungumza na msamamizi wa kituo hichi pamoja na Polisi ambae ni
msamimizi mkuu wote walikiri kuwa sanduku limeibwa na kwa pamoja wote
tulikubaliana kuwa sanduku liliibwa na mtu ambae alikuja na kulipora
japo watu walikuwa wamekaa hapa hapa akatokomea nalo", amesema Salum.
Pamoja
na hayo, Salum Mwalimu ameendelea kwa kusema "baada ya dakika kama 10
hivi sanduku likarudishwa. Sasa kinachonishangaza ni kwamba Polisi na
Tume wanasema uchaguzi uendelee. Yaani kura zimeibwa na Polisi wapo na
kuna mpaka wa vyeo vya juu kutoka katika Mkoa wa kipolisi Kinondoni"
Aidha,
Mkuu wa kituo hicho alipofuatwa na muandishi kuulizwa juu ya sakata
hilo alidai aruhusiwe kuongea jambo lolote kwa kuwa yeye hana mamlaka ya
kuongea.
0 comments:
Chapisha Maoni