Mke
wa aliyewahi kuwa mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, Jesca Kishoa,
amemtaja mumewe kuwa ni mtu aliyeingia kundi la wanasiasa wasio na
msimamo.
Kishoya amesema wakati wote mumewe amekuwa na msimamo usioyumba lakini anashangazwa kaingia katika mtego mbovu.
"Bado
naamini kuwa Chadema ni mahali sahihi kabisa ambapo siwezi kufikiri
siku moja nitatoka, hivyo siyumbi kwa hilo na wanaonipigia simu
watambue hilo," amesema Kishoya
Amesema
taarifa za mumewe kujiondoa Chadema amezipata kupitia vyombo vya habari
akiwa Dodoma kwenye kampeni za udiwani lakini alimpigia wakazungumza
sana na bado hakumpa sababu zilizoshiba za kuondoka kwake.
Hata
hivyo amepinga madai ya Kafulila kuwa anaondoka upinzani kwa sababu ya
upinzani kushindwa kusimamia ajenda ya ufisadi badala yake akasema ana
mambo yake.
"Wanasiasa
ambao hawana misimamo ndiyo husingizia vitu hivyo, siamini kama maneno
yale yalitoka rohoni mwake, CCM siyo mahali sahihi kwa kuzungumzia mambo
ya ufisadi hata kidogo, "
Mbuge
huyo amesema wakati wote katika maisha yao mumewe amekuwa ni muumini
mzuri wa kuhubiri habari za ufisadi ikiwemo pale alipotoa maisha yake
kuhusu sakata la Escrow.
0 comments:
Chapisha Maoni