Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Vicent
Mashinji amekanusha habari za kwamba anahamia Chama cha Mapinduzi na
kusema kwamba yeye siyo mtu wa kuamini kwenye zidumu fikra za Mwenyekiti
bali nguvu ya mamlaka ya umma.
Mashinji
amesema kwamba yeye siyo mjamaa bali ni mlengo wa kipepari hivyo
amewataka wananchi wawe na amani kuhusu hizo taarifa za yeye kuhamia CCM
si za ukweli.
"Napokea
simu nyingi eti nahamia CCM, mi si Mjamaa. Mi ni mlengo wa kibepari.
Siamini kwenye “zidumu fikra za mwenyekiti” Ninaamini katika “nguvu na
mamlaka ya umma”. Naomba ndugu zangu muwe na amani kabisa" Mashinji.
Dkt Mashinji ameongza kwamba "Nitaendelea kutumikia CHADEMA kwa makini na kutimiza ndoto za watanzania".
0 comments:
Chapisha Maoni