Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla amefunguka na
kukilalamikia moja ya chombo cha habari na kusema kuwa kimepanga
kumchafua na kumchonganisha na Rais Magufuli na kudai anatambua kwa
hatua anazochukia watu wa namna hiyo watakuwa wengi
Kigwangalla
amesema kuwa chombo cha habari hicho kimemsema kuwa amepingana na Rais
Magufuli kwa kuruhusu mifugo iingizwe ndani ya hifadhi zote za Taifa
ikiwepo Serengeti kitu ambacho yeye hakusema hivyo.
"Najua
lengo ni kunichonganisha na Mamlaka iliyoniteua. Najua watu wa aina hii
watakuwa wengi sana kwa sasa sababu nimegusa maslahi ya watu wengi sana
kwa maamuzi magumu niliyofanya siku za karibuni, kuanzia kwenye suala
la kufuta mchakato wa vibali vya uwindaji, kupambana na majangili hadi
kuanza mchakato wa kurudisha kwenye umiliki wa Serikali hoteli zote
zilizokuwa za Serikali kupitia Shirika letu la Tanzania 'Tourist
Corporation' kwa kushindwa kwao kuziendesha kwa tija kwenye sekta ya
utalii" alisema Kigwangalla
Waziri
huyo amesema kuwa kabla ya kukikuchukulia hatua chombo hicho cha habari
ameamua kusema na kuweka wazi kile alichokisema na kudai endapo
wasiporekebisha hiyo taarifa atachukua hatua zaidi.
"Binafsi
nimekisamehe chombo hiki, lakini ili wajifunze kuwa mimi si mtu wa
kuchezea waombe radhi haraka kabla sijawaburuza kwa Waziri wa Habari,
Dr. Mwakyembe, nikiwa na ushahidi wangu ili achukue hatua stahiki"
aliandika Kigwangalla
Kigwangalla
anasema alisitisha oparesheni iliyoendeshwa kwenye eneo la Kilomita 5
nje ya mpaka wa Serengeti ndani ya Pori la Loliondo ambapo kuna mgogoro
wa ardhi
"Mimi
nilisitisha operesheni iliyoendeshwa kwenye eneo la km 5 nje ya mpaka
wa Serengeti ndani ya Pori Tengefu la Loliondo kwenye ardhi yenye
mgogoro, na ni baada ya kupokea taarifa za ukiukwaji wa Sheria za
vijiji, na uwepo wa minong'ono kwamba Serikali iliendesha 'operation'
hiyo Kwa kutekeleza matakwa ya muwekezaji. Jambo nililoona linaichafua
Serikali na Mhe. Rais. Nilifanya hivyo sababu najua kuna Kamati ya Mhe.
Waziri Mkuu inashughulikia suala la mgogoro wa pori Tengefu la Loliondo"
alisisitiza Kigwangalla
0 comments:
Chapisha Maoni