Rais
John Magufuli amelitaka shirika la utangazaji la TBC, kutoa taarifa
sahihi kwa watanzania bila kujali vyama vyao, dini zao wala makabila
yao.
Pia
Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
MichezoHarrison Mwakyembe aliyekuwepo katika ziara hiyo kuuangalia
mkataba kati ya TBC na Star Times na kuchukua hatua zinazostahili endapo
itabainika kuwa mkataba huo hauna manufaa.
Magufuli
ameyasema hayo jana alipotembelea ofisi za Shirika hilo na kuwataka
wafanyakazi wa TBC kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na ubunifu wa hali
ya juu ili matangazo ya chombo hicho cha Taifa yawavutie Watanzania
wengi, na kiwe chombo kinachoongoza nchini.
Magufuli
ambaye hivi karibuni ametoa Sh3bilioni kwa ajili ya kuisaidia TBC
amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Dk Ayub Rioba kutumia fedha
hizo kutatua matatizo ya uhaba na uchakavu wa vifaa vya uzalishaji wa
vipindi na urushaji wa matangazo, kununua vyombo vya usafiri na kufanya
ukarabati wa majengo.
Kuhusu
maslahi ya wafanyakazi amewahakikishia kuwa Serikali itaboresha stahili
zao kwa mujibu wa utaratibu uliopo na papohapo amemuagiza Dkt. Rioba
kulipa mara moja malimbikizo ya posho zote ambazo wafanyakazi hao
wanadai kuanzia Oktoba 2016, zilizofikia Sh3.2bilioni.
“Msemaji
wa Serikali mkubwa ni TBC1 na Redio ya Taifa, nyinyi hamuwezi mkawa
kama vyombo vingine ambavyo vina malengo yao ya kufanya biashara, nyinyi
kazi yenu ni kutoa taarifa sahihi kwa Watanzania bila kubagua vyama
vyao, bila kubagua dini zao, bila kubagua makabila yao, huo ndio uwe
msimamo mkuu.
“Mmetoa
mchango mkubwa sana kwenye Taifa hili, hilo ni lazima niseme, hata
vipindi vyenu ukiviangalia ni vizuri vinaeleza mpaka maisha ya vijijini,
na mimi ni shabiki mkubwa sana wa TBC, lakini tatizo lenu mnashindwa
kwenda na wakati wa sasa.” amesisitiza Rais
0 comments:
Chapisha Maoni