Mbunge
wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa
huru kwa dhamana na kutakiwa kuripoti siku ya Jumanne saa tatu asubuhi
kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI) jijini Dar es
Salaam.
Mwanasheria
wa Zitto Kabwe amesema kuwa mpaka sasa mteja wake anatuhumiwa kwa
makosa mawili tofauti likiwepo kuchapisha taarifa kinyume cha sheria ya
mitandao lakini kosa jingine ni kutoa takwimu za uongo kinyume na
kifungu cha 37 (5) cha sheria ya takwimu ya mwaka 2015 hivyo mwanasheria
anasema Zitto Kabwe amehojiwa na kutoa maelezo yake hivyo wanasubiri
kujua kama watakwenda mahakamani.
Kwa
upande wake Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwa sasa wanasubiri kuona
wanapelekwa mahakamani ili waweze kujadiliana huko na kusema kama wao
kuna makosa ambayo wanayaona kwake sehemu pekee ambayo wanaweza kwenda
kufafanua vizuri ni mahakamani na kudai kuwa kama asingekamatwa
angeshangaa kwa kuwa tayari Rais alikuwa ameshatoa agizo.
"Tunasubiri
ni lini watatupeleka mahakamani kwa ajili ya kutetea masuala ambayo
tumezungumza lakini ya ziada ni kama ambavyo Mwanasheria amezungumza kwa
hapa ni makosa mawili ya Sheria ya Takwimu na Sheria ya makosa ya
mitandao, wananchama waendelee kuwa watulivu tu kwa sababu kila mtu
alitarajia kuwa tutakamatwa kwa kuwa Rais alisema kuwa nikamatwe hivyo
tusingekamatwa ningeshangaa, la ziada ni kwamba tusubiri mahakamani
itakuaje" alisisitiza Zitto Kabwe
Mbali
na hilo kiongozi huyo wa ACT Wazalendo amewataka wanachama pamoja na
viongozi wa chama hicho kuendelea na harakati za uchaguzi mdogo wa
udiwani na kusema endapo wakishinda katika uchaguzi huo ni kitu ambacho
kitakuwa faraja kwao.
0 comments:
Chapisha Maoni