Jubilee
wameiga kaulimbiu ya kampeni ya muungano wa Nasa baada ya kikundi cha
wanawake kutoa wito wa kujizuia kufanya ngono hadi pale
watakapokamilisha kumsimika Uhuru Kenya kuwa rais.
“Hakuna
ngono hadi baada ya uchaguzi” ni kauli ya hamasa iliyoanzishwa na
mgombea urais kwa tiketi ya Nasa, Raila Odinga kwamba wakati wa vita
wanaume huwa hawalali na wake zao. Kauli hiyo ilikuwa maarufu kipindi
cha kuelekea uchaguzi wa Agosti 8.
“Agosti
8 inakuja; itakuwa siku ya kihistoria na hakuna mtu atakayeachwa bila
kupiga kura. Wanaume watalala nje. Siku itakapofika, hakuna mwanamume
kulala na mkewe,” alikuwa akisema.
“Mnapokwenda vitani, ngono ni mkosi,” Odinga alinukuriwa akisema Juni.
Safari
hii kikundi cha wanawake nchini kimetoa rai ngono ipigwe marufuku
kuelekea uchaguzi mkuu wa marudio ambao umeamriwa na Mahakama ya Juu.
Ingawa
sintofahamu imetawala uchaguzi huo uliopangwa Oktoba 26, wanawake
katika mji wa Nyeri katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano
walisema hawatashiriki ngono na waume zao hadi Uhuru Kenyatta
atakapoapishwa kuwa rais kwa muhula wa pili.
Kiongozi
wa kikundi hicho, Rahab Mukami, ambaye ni mwakilishi wa wanawake
alisema wanawake wameimarisha kampeni kuhakikisha Kenyatta anashinda.
Tume
Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imesisitiza kwamba uchaguzi
utafanyika kama ulivyopangwa licha ya mgomo ulioitishwa na Odinga wa
National Super Alliance (Nasa).
Nasa
wametoa wito kwa wafuasi wao kufanya maandamano makubwa siku ya
uchaguzi. Mara kadhaa wafuasi wao wamepambana na polisi katika mitaa
ambayo muungano huo ni ngome zao.
0 comments:
Chapisha Maoni