Daktari
bingwa wa uchunguzi wa magonjwa ya binadamu na vifo vyenye kutia shaka,
Innocent Mosha kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili ameieleza Mahakama
Kuu alichobaini baada ya kuufanyia uchunguzi mwili wa msanii wa fani ya
uigizaji wa filamu nchini, Steven Kanumba.
Dk
Mosha ambaye ni shahidi wa nne wa upande wa mashtaka katika kesi ya
kuua bila ya kukusudia inayomkabili msanii wa fani hiyo, Elizabeth
Michael maarufu Lulu amesema walipofungua fuvu walibaini ubongo wa
Kanumba ulikuwa umevimba.
Lulu anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
Katika
ushahidi wake leo Jumatatu Oktoba 23,2017, Dk Mosha akiongozwa na
Wakili wa Serikali, Faraja George mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Samu
Rumanyika ameeleza akiwa kazini alipewa maagizo kuwa anatakiwa kuufanyia
uchunguzi mwili uliokuwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili.
Shahidi
huyo amesema katika uchunguzi wa mwili wa Kanumba alibaini kuwepo
uvimbe sehemu ya nyuma kwenye ubongo na walipofungua fuvu walibaini
ubongo ulikuwa umevimba.
Dk
Mosha alipoulizwa na wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala juu ya sampuli
walizopeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusu hali ya kilevi katika
mwili wa Kanumba, amesema hakuwahi kufahamu matokeo ya uchunguzi.
Pia, amesema hafahamu kama Kanumba alijigonga ukutani kwa kuwa hakuwepo eneo la tukio.
0 comments:
Chapisha Maoni