Nikamkabidhi
msichana hati yangu ya kusafiria cha kwanza akanitazama machoni, kisha
hati yangu ya kusafiria akaiweka kwenye mashine inayotoa ripoti kwenye
kioo kikubwa cha ‘computer’.Askari anaye kagua akaanza kazi yake ya
kukipitisha kifaa chake kuanzia miguuni, msichana akanitazama kwa macho
makali kisha akatazama tena kwenye kioo cha kumputer yake, nikatazama
pembeni na kuwaona askari wawili walio shika mbwa wakubwa weusi wakianza
kunisogelea, huku wakiwa na bubduki zao mikononi, kifaa cha ukaguzi
kikaanza kutoa mlio wa kelele huku kikiwaka taa nyekundu kilipo fika
maeneo ya shingoni
Endelea
“vua cheni yako”
Askari
anaye nikagua aliniambia na kunifanya niivue cheni, niliyo ivaa
shingoni mwangu.Akaendelea kukipitisha kifaa chake kwenye mgongo hadi
chini kwenye miguu,
“safari njema”
Dada
aliyekuwa anaikagua hati yangu ya kusafiria alizungumza huku
akinikabidhi hati yangu ya kusafiria, huku usoni mwake akiwa ameachia
tabasamu pana lililo pendezeshwa na mwanya wake mwembamba.
“asante na wewe pia kazi njema”
Nikapita
kwenye kizuizi na kuwafanya sashah na rajiti kushusha pumzi nyingi
kwani walihisi kwamba tayari nimeingia kwenye mikono ya askari,
tukaingia ndani ya ndege, cha kushukuru mungu, siti zetu tatu zipo
sehemu mmoja, hatukukaa hata dakika nyingi, rubani akatuomba tufunge
mikanda yetu kwani ndege itajiandaa kuruka muda sio mrefu.Ndani ya
dakika kadhaa tukaanza kuiacha ardhi ya nchini kenya
“eddy” rajiti aliniita
“naam”
“unajua kwamba unaonekana tofauti sana”
Alizungumza kwa sauti ndogo
“kweli?”
“ndio, umekuwa bonge la handsome”
“mmmmm”
“kweli vile”
“jamani acheni kelele watu wamelala” sashah alizungumza
“ahaaa shauri yao, bwana”
Masaa
yakazidi kusongo mbele, na ndege yetu ikatua baadhi ya nchi ambapo,
baadhi ya abiria walishuka na kupanda abaria wengine na safari
ikaendelea.Tukafika nchini iraq, majira ya saa moja saa tisa alasiri
huku sote tukiwa tumechoka kwa uchovu wa kukaa kwenye ndege takribani
masaa kumi na tano, kutokana hatukuwa na mizigo tukawahi kupanga mstari
wa kutokea sehemu ya kukaguliwa, huku moyoni mwangu nikiwa ni naomba
sana nisiweze kushtukiwa kwa lolote, na nikafanikiwa kutoka njee ya
uwanja wa ndege pasipo mtu yoyote kunistukia kwamba nimevalia sura
bandia,
Sikuwa
na sehemu yoyoote ninayo itambua na wenyeji wangu wakubwa ni sashah na
rajit.Tukapanda kwenye taksi mojawapo iliyopo kwenye maegesho ya uwanja
wa ndege na sashah akazungumza kwa lugha ya kiarabu na dereva tuliye
mkuta ndani ya teksi hii, tukafika kwenye moja ya hotel kubwa iliyo
andikwa kwa maandishi ya kiarabu na kila kitu ambacho wanakizungumza
shasha na watu wengine, sikuweza kukifahamu kutokana siitamui lugha ya
kiarabu
Sashah
akamaliza kuzungumza, na wahudumu na akakabidhiwa funguo moja,
akatufwata sehemu tulipo simama na rajit, tukaingia kwenye lifti iliyo
tupeleka hadi ghorofa ya sita, na tukaingia kwenye chumba ambacho sashah
alikodisha
“eddy utakaa hapa siku mbili, ili uyazoee mazingira kisha tutaelekea makao makuu”
Sashah alizungumza
“na nyinyi munakwenda wapi?”
“sisi,
tunakwenda kufwatilia mambo muhimu, kwa ajili ya kazi zetu, kikubwa ni
wewe kuwa makini katika hili eneo.Tumekulipia chakula kila mahitaji
utakayo yahitaji tumegharamia”
“sasa jam….”
“eddy
hapo hakuna cha sasa kikubwa ni wewe kuwa makini, usipende kujitokeza
tokeza kwa watu kwani watu wa huku hawana huruma, wana roho za
kinyama.Yaani ukitembea sana wewe mwisho wako ni kule chini kwenye
sehemu ya chakula”
“sawa nimewaelewa, je nikihitaji hudumu ya kuwapigia wahudumu wa hii hoteli?”
“kuna
kitabu pale juu ya meza kwenye ile simu basi utaweza kuitumia hiyo
sawa, na kabla sijasahau chukua hizi cuppon ukienda kuchukua chakula
unaonyesha, zipo za ana mbili, moja ya chakula na nyingine ya
kinywaji.Ukizipoteza baba utashinda njaa hizi siku mbili”
“powa”
Sashah
na rajit wakaondoka na kuniacha nikiwa nimesimama, nikawasindikiza kwa
macho hadi walipo funga mlango ndipo na mimi nikapiga hatua hadi kweye
mlango na kuufunga kabisha kwa funguo na kurudi kujilaza kwenye kitanda
kikubwa kilichomo ndani ya hii hotel.Nikanyanyuka na kusimama mbele ya
kioo kikubwa na kujitazama sura yangu, kusema kweli nimebadilika kwa
kiasi kikubwa
Nikavua
suti niliyo ivaa na kuingia bafuni, nikaoga huku kichwani kwangu nikiwa
nimejawa na mawazo yaliyo ambatana na maswali mengi juu ya wapi alipo
mama yangu,
“hii ni nafasi yangu ya mwisho kupambana na mzee godwin, nilazima nimuue kwa mkono wangu mimi mwenyewe”
Nilizungumza
huku nikiwa nimekiinamisha kichwa chwangu kwenye ukuta, huku
nikiyatazama maji yanayo tiririka na kuingia kwenye kijishimo kidogo
“ilipo fikia inatosha”
Nilizungumza
huku nikishusha pumzi nyingi, nikamaliza kuoga na kurudi chumbani, saa
ya ukutani inanionyesha inakwenda majira ya saa kumi na moja kasoro
jioni.Nikapanda kitandani, kutokana na uchovu mwingi nikajikuta taratibu
nikiwanza kusinzia hadi usingizi ukapitia kabisa
Nikastuka
kutoka usingizini, na macho yangu yakakumbana na giza, nikashuka
kitandani na kupiga hatua za ungalifu hadi sehemu ilipo swichi,
nikawasha taa cha kwanza kukitazama ndani ya chumba ni saa iliyopo
ukutani na kukuta ikionyesha ni saa nne na dakika kumi na nane usiku,
nikavaa nguo zangu na kutoka nje ya chumba, nikashuka chini sehemu ya
watu kujipatia chakula
Nikaa
kweny moja ya meza, muhudumu akanifwata na kuniuliza kwa lugha
kingereza ninatumia chakula gani, kati ya vyakula vilivyo orodheshwa
kwenye menyu yao.Kila chakula ambacho ninakisoma kwangu ni kigeni,
nikaamua kuweka tiki kwenye chakula ambacho niliona jina lake
linanipendeza, kinywaji nilicho kielewa kikubwa ni maji tuu ndio niliyo
amua kuyawekea tiki
Muhudumu
akaondoka na baada ya muda akarudi akiwa na chakula nilicho muagiza,
nikajikuta nikishusha pumzi nyingi kwani chakula nilicho kiagiza, ni
konokono wakiwa wamechemshwa vizuri huku wakiwa wamepambwa na nyanya
zilizo katwa vizuri na kuwekwa pembezoni mwa shahani hiyo
“mmmm, bora nirudi bongo, kwa staili hii”
Nikawatazama
watu wengine kwenye meza zao, kila mmoja yupo bize na mambo yake, jamaa
mmoja aliye kaa pembeni yangu nikamuona akiwekewa chakula kama changu
na muhudumu aliye muagiza, bila hata ya kusita akaanza kutafuna nyama za
konokono hao huku akishushia na soda.Kwa jinsi jamaa anavyo wala
nikajikuta nikianza kujihisi kichefuchefu kwa mbali, kila ninapo
watazama konokono wangu ndovyo jinsi kichefuchefu kinavyo ongezeka na
kujikuta nikisimama na kumsimamisha muhudumu mmoja
“where is toilet”(choo kipo wapi)
Nilizungumza
huku kiganja cha mkono wangu wa kulia kikiwa mdomoni mwangu kuzuia
kutapika, muudumu akanionyesha kwa kidole mlango wa kuelekea chooni,
nikaanza kupiga hatua za kwenda kuufwata mlango huku ninatizama chini
kwa bahati mbaya nikamgoga msichana mmoja mmrefu aliye nipa mgongo, na
pochi yake ikaanguka
“so….”
Sikuweza
hata kuimalizia samahani yangu, tayari kechefuchefu kilikolea, nikazidi
kutembea kuelekea chooni, ila kwa msonyo alio uachia huyu dada
ikanilazimu kugeuza kichwa kumtazama huku nikiwa ninatembea, macho yangu
yakamshuhudia dorecy akimalizia kunyanyuka huku akiwa ameshika kipochi
chake kilicho anguka, kutokana na hali mbaya niliyo nayo sikuwa na budi
kuingia chooni.Nikasimama kwenye moja ya sinki la kunawia mikono na
kuanza kutapika, dakika tato mfululizo nikajikuta ninatapika hadi
chakula nilicho kula ndani ya ndege.
Tumbo
likaanza kunisokota, sikujua hata ni kitu gani kilicho nikumba kwa
dakika chache hizi, ikanilazimu kujisaidia haja kubwa, kidogo nikapata
nafuu ya tumbo kuniuma.Nikajiwek sawa na kunawa mikono yangu, nilipo
hakikisha ninaonekana vizuri nikafungua mlango na kumkuta yule jamaa
aliyekuwa anakula konokono akiwa amesimama juu ya meza huku mkoni mwake
akiwa na bomu la kurusha kwa mkono, watu wote wakanza hulala chini huku
wakipiga kelele, jamaa akafungua kikoti chake alicho kivaa na
nikamshuhudia akiwa amejifunga mabomu mengine makubwa kama maane na
akaanza kuzungumza kwa sauti ya juu kwa lugha ya kiarabu na neno nililo
lielewa ni moja tu
“walha wakhbar”
Kisha
akalirusha juu bomu la mkoni, alilokuwa amelishika, huku mabomu mengine
aliyo yavaa mwilini mwake yakisoma zero nyingi zinazo onekana kwa rangi
nyekundu
*****sory madam*****(58)
Fumba
na kufumbua, nikajikuta nikiwa nimerushwa na kurudishwa nyuma ndani ya
choo nilipo tokea, huku sauti kubwa ya mlipuko wa bomu ikisikika,
sikujua hata nini kufanya kwani akili yangu ikakakosa maamuzi ya hataka
ya kuamua, hadi ninaanza kupata chakufanya, tayari nimesha chelewa kwa
maana kuta za choo zilisha anza kuporomoka na kusababisha upenyo mdogo
sana.Nikazidi kuchanganyikiwa kiasi kwamba sikujua ni nini niweze, gafla
nikashuhuda kifusi kikubwa cha mchanga kikilifunikia sehemu zima la
chooni na taratibu nikaanza kupoteza pumzi na kulegea, na giza jingi
likanitawala machoni mwangu
***
Nikaanza
kuhisi kitu kikinistua kwenye kifua change, sikuweza kuelewa mapema ni
vitu gani.Kelele za watu za watu mchanganyiko zikazidi kunipa hamasa ya
kutamani kuona ni kitu gani kinacho endelea kwenye maisha yangu kwa
wakati huu.Haikuwa rahisi sana kama ninavyo hitaji mimi kuwa, kwani kila
kitu kinacho endelea kwenye ulimwengu huu niliopo ni chatofuti sana, na
sijawahi kukiona hata siku moja mbele ya maisha yangu.Mwanga mkali
ukasimama mbele yangu, na kundi kubwa sana la watu walio valia mavazi
meupe yanayo ng’aa sana, wakiwa wapo kwenye marika tofauti kuanzi watoto
wadogo hadi wakubwa, wote wakiwa wapo kwenye jinsia tofauti
nikimaanisha jinsia ya kiume naya kike.
Kila
niliye mtazama akaanza kutingisha kichwa, akionyesha kukaataa kitu na
sikujua ni kitu gani ambacho anakikata, wakaanza kuninyooshea mikono ya
kuniomba nirudi ninapotoka, sikujua ni wapi nilipo taoka kutokana sehemu
nzima niliyo simama imetawaliwa na mwanga mweupe mtupu ambao sikuweza
kuona ni wapi popote zaidi ya hawa watu walio simama mbele yangu
“eddy, wakati wako bado.Rudi”
Sauti
nzito ya kutetemesha ilisikika masikioni mwangu, na gafla nikisikia
mstuko mkali kwenye kifua change ulio nifanya nistuke na kukaa kitako
huku ninahema sana, na jasho jingi likiwa linanimwagika mwilini
mwangu.Watu waliopo pembeni yangu walio valia mavazi ya kijana huku sura
zao wamezifunika kwa vitambaa vinavyo fanana na mavazi yao,
wajanirdusha haraka kulala kwenye kitanda.Nikaanza kuminyanana nao huku
nikiomba waniachie
“niachieni nyinyi, mimi mzima sijafaaaa”
Nilizungumza
kwa sauti ya juu huku nikijitahidi kunyanyuka, ila wakazidi
kunishikilia na kunikandamiza nisirudi kukaa, nikamuona dada mmoja
akichukua sindano na kuichoma kwenye kwenye kichupa kidogo na kuvuta
dawa nyingi kwa haraka
“haaaaa, haaa unataka kuniua eheeee, kudadadeki nitakuua kwanza wewe”
Nilizungumza
huku macho yangu nikiwa nimemtumbulia dada mwenye sindano, ila wezake
wakajitahidi kunishika kwa nguvu zao zote, na nikamshuhudia dada
akiichoma sindano kwenye mkono wangu wa kushoto, na kadri jinsi
anavyoisukuma dawa ndivyo jinsi na mimi nilivyoanza kupoteza nguvu na
usingizi mzito ukaanza kunitawala kila nilivyo jaribu kufumbua macho
yangu nikashindwa kabisa
***
Nikastuka
na kukuta, mashine ndogo ikiwa pembeni yangu ikionyesha mishale mishale
ambayo imepinda panda, kujichunguza vizuri nikajikuta nikiwa
nimevalishwa kitu kilicho funika pua yangu na mdomo wangu, sikuwa na
nguvu za kufanya kitu chochote zaidi ya kuendelea kujilaza kwenye
kitanda nilicho lazwa.Taa mbili nyeupe za chumba hichi hazikunipa uwezo
wa kugudua kama huu ni usiku au mchana.Nikajaribu kujiinua ila
nikashindwa na kuendelea kulala kitandani
Baada ya muda kidogo ukaingia nesi akiwa amebeba kisinia chenye sindano, pamoja na vichupa viwili vyenye rangi tofauti tofauti
“unajisikiaje?” aliniuliza kwa sauti ya chini iliyo jaa upole mwingi
“vizuri”
“vizuri, usiwe na wasi wasi upo sehemu salama na utapona sawa kaka”
Alizungumza huku akivaa gloves nyeupe kwenye mikono yake
“kwani hapa nilipo nipo wapi?”
“upo hospitali, ila kwa sasa tunajitahidi kukushuhulikie ili uweze kupona haraka”
“kwani hapa ni tanzania?”
“hapana hapa ni iraq”
“mbona unazungumza kiswahili kizuri”
Nilimuuliza
huyu nesi mwenye asili ya kiarabu, akatabasamu na kuvuta dawa kidogo
kwenye kichupa, kwa kutumia sindano kisha akachukua pamba na kuipaka
dawa kidogo na kunipaka kwenye mkono wa kulia sehemu ya kikunjio,
akanichoma sindano yanye dawa
“pole eheee”
Alizungumza kwa sauti yepesi sana iliyo jaa upendo na upole
“asante”
“ikifika asubuhi nitakuja kukuchoma sindano ya kutuliza maumivu”
“sawa”
Akakusanya
kila kilicho chake na kutoka ndani ya chumba.Masaa yakazidi kwenye na
kuzidi kukatika taratibu huku nikiwa nimesongwa na msongamano wa mawazo
nikijaribu kuvuta kumbukumbu za hapa kufika hospitali ila sikukumbuka
kitu cha aina yoyote, jina ambalo ninalo kichwani mwangu ni tanzania,
pamoja na lugha yangu ya kiswahili ambayo kwangu ndio lugha ya taifa
Wakaingi
madaktari wawili wote wakiwa waarabu, wakanisogelea hadi kwenye kitanda
nilicho lala na kuanza kuzungumza huku mmoja akianza kunishika
mashavuni na kuniminya minya.Wakaendelea kuzungumza huku mmoja akiandika
kwenye kijikitabu kidogo alicho kuja nacho.Mmoja akanifunua shuka na
kumuonyesha mwenye kijikitabu mkononi sehemu ya mguu wangu, mapigo ya
moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kuuona mguu wangu wa kulia ukiwa
umefungwa kitu kikubwa cheupe.Akaingia nesi wa jana usiku na kusimama
pembeni ya madaktari hawa, huku akiwa ameshika kisinia chake cha jana
usiku.Nikaanza kumuona nesi akitingisha kichwa akionekana kukataa
mazungumzo ya madaktari hao
Wakaanza
kubishana, na sikujua ni kitu gani wanacho bishana.Hadi ikafikia
daktari mmoja wa aliyekuwa anazungumza na mwenzake anaandika akataka
kumzaba kibaa nesi huyo, ila mwenzake akakataa na kumtoa nje, kuepusha
ugomvi kutokea ndani ya chumba hichi.Nesi akaanza kuzunguka ndani ya
chumba huku akimwagikwa na machozi na kuzidi kunichanganya kwani sikujua
ni kitu gani kinacho mwaga machozi kwa kiasi hichi.
“kuna nini?”
Nilimuuliza
na kumfanya asimame na kunitazama, akautazama mlango na kwenda kuufunga
kwa ndani, kisha akarudi na kukaa pembeni yangu huku akinifunika na
shuka
“eti nesi, kuna nini?”
Nilimuuliza kwa sauti ya upole iliyo jaa huzuni, akanitazama na machozi yakazidi kumwagika kiasi cha kuzidi kunichanganya mimi
“watu wa huku, wana roho mbaya sana pale wanapo waona watu wenye ngozi yeupe”
Alizungumza huku akijifuta machozi yanayo mwagika kwa kutumia kiganja chake
“kwa nini?”
Akanitazama kwa umakini na kwamacho yaliyo jaa huzuni kiasi cha kunifanya nihisi kuna jambo baya ila sikujua ni nini
“kiufupi hawawapendi watu weusi, ndio maana wanafanya mpango wa kukukata huu mguu wako ulio vunjika”
Nilijihisi
moyoni mwangu kama nimepigwa shoti ya umeme, kila nilivyo mtazama nesi
sikujua nizungumze nini.Machozi yakaanza kunimwagika kama maji,
“usilie, nitahakikisha unapona na hakuna mtu anaye weza kukufaniyia ukatili kama huo”
“kwani umekatika?” nilimuuliza kwa sauti ya upole sana huku nikiendelea kulia
“hapana haujakatika, umefunjika mara mbili, ila nashangaa ni kwanini hapa wanapanga kuukata”
“ila
usilie, nipo radhi nipoteze kila kitu kwangu, ila si kukubali kuuona
ubaguzi wa rangi kama huu.Kwa maana wakiukata kinacho fwatia hapa ni
wewe kupelekwa katika kambi ya walemavu iliyopo bangdad na kila siku
hiyo kambi, walemavu wanakufa kwa njaa kali na mateso makali, na mbaya
zaidi wengi wanao pelekwa kule ni wale ambao si raia wa nchi hii”
Maneno ya nesi yakazidi kuniogopesha na kuendelea kunipa wasiwasi mkubwa ulio zidi kunimwaga machozi yangu.
“jikaze
usilie, ngoja nikuchome sindano ya kutuliza maumivu na kukausha
kidonda.Wakikuletea chakula tafadhali usile hadi nikuletee mimi”
“sawa”
“wanaweza kukupa sumu, ufe bure mtoto wa watu bila ya sababu maalumu”
Nesi alizungumza na kuendelea kunichoma sindano alizo niambia,
“sasa
hivi ninatoka, kazidi ninakwenda nyumbani kukuandalia chakula, hadi saa
sita nitakuwa nimesha rudi kukuletea chakula na nikija nitakuja
tuzungumze mengi.Ila vumilia njaa yako, usile chakula wala kunywa maji
yoyote utakayo letewa na mtu wa aina yoyote sawa”
“sawa, nashukuru kwa msaada wako nesi”
“hata wewe nashukuru kwa uelewa wako, niite neshi phidaya”
“naitwa eddy”
“mungu mkubwa utapona na vua hiyo mashine”
Nikakivua
kifaa nilicho kuwa nimevalishwa kwenye uso kisaha, nesi phidaya
akaondoka na kila kitu chake, baada ya muda kidogo akaingia nesi akiwa
amebeba sahani nyenye chakula pamoja na maji kwenye glasi, akaviweka
pembeni ya meza yangu na kunitazama usoni.Akawa anatamani kuzungumza na
mimi ila anashindwa na nikahisi lugha zetu zipo tofauti sana.Akanza
kunionyesha kivitendo kwamba chakula kipo mezani ninaweza kula, na mimi
nikamjibu kivitendo kwamba nitakula, akatoka na kuniachia chakula
mezani. Harufu ya chakula ikazidi kunitamanisha kuweza kukila kwani
inavutia sana, ila kila nilipo jaribu kukumbuka maneno ya nesi phidaya
nilijikuta nikuwa ninakidharau
Baada ya muda mrefu kidogo nesi phidaya akarudi akiwa emeshika mfuko mweupe wenye vyombo,
“nani kakuletea chakula?”
“nesi mmoja mfupi, mwarabu”
Nesi phidaya akaachia msunyo mkali baada ya kumuambia nesi aliye niletea chakula hicho
“ndio wale wale”
Akakisogeza chakula nilicho letewa akaniwekea chakula chake mezezani, akaanza kuninywesha taratibu uji alio uweka kwenye kikombe
“watu wa huku hawana ubinadamu, ndio maana kila siku wanakazi ya kujitoa muhanga na mabomu yao”
“hivi ni kwa nini?”
“uchizi
tu ndio unao wasumbua, kuna wanao amini kwamba ukijitoa muhanga, mbele
za watu mbinguni utaingia moja kwa moja wakati ni uongo mtupu”
“hivi unakumbuka kitu chochote cha nyuma?”
“hapana”
“ona sasa, wamekuchoma sindano ya kukupotezea kumbu kumbu, ndio maana nakuambia watu wa huku hawana maana”
“wamenichoma sindano?”
“ndio,
na kuna kitu kinacho endelea, na ile siku ya oparesheni kama nisinge
kuwepo ninaimani wangekumalizia, nikutokana katika watu walio okolewa
wakiwa hai kwenye lile jingo wewe ni mmoja wao na idadi kubwa ya waarabu
walikufa pale”
“kwenye jengo, jengo gani?”
“usiwe na haraka, hapa itabidi nifanye mpango wa kukutorosha la sivyo watakupoteza”
Maneno
ya nesi phidaya yakazidi kunipotezea imani moyoni mwangu na kunijaza
moyo wa woga kwani imani ya kuwaamini madaktari wengine ikaanza
kunipotea moyoni mwangu.Nesi phidaya akamaliza kunilisha chakula alicho
niletea na kunihaidi atarudi usiku kisha akaondoka zake
***
Masaa
yakazidi kusonga, huku moyoni mwangu nikiomba sana nesi phidaya atokee
aje kunisaidia kwa maana kila daktari kwangu sikuweza kumuamini, kila
nilipojaribu kuvuta subira sikuweza kumuona nesi phidaya akiingia kwenye
chumba change, mlango ukafunguliwa na kujikuta nikianza kutabasamu,
macho yangu yakiwa na shauku ya kuweza kumuona nesi phidaya.Nikashangaa
kuwaona wale madaktari wa asubuhi wakiingia na kusimama pembeni yangu
Mmoja
akafungua kitabu chake kilicho andikwa na maandishi ambayo akanionyesha
na sikumuelewa ni maandishi ya lugha gani, akaniandikia tarehe kwenye
kijikitabu chake na kuniambia kwamba hii ni tarehe ya leo, kish
akaniandikia tarehe nyingine ambayo ni siku inayo fwata.Kisha akachora
kijimguu na kukiwekea alama ya ‘x’ akiashiria kwamba kesho ndio siku ya
mimi kukatwa mguu wangu.Alipo maliza kunionyesha kwa ishara wakatoka
huku wakiwa wanacheka sana.
Hadi
kunapambazuka sikuweza kumuona nesi phidaya, hali ya hatari ikaanza
kunijia kichwani mwangu na kuhisi nesi phidaya anaweza kuwa amekutwa na
matatizo, mlango ukafunguliwa na wakaingia manesi wawili pamoja na
madaktari wale wawili.Wakaanza kufungua kitandana na kukishusha chini
kidogo hadi kikafikia usawa mzuri wa kuweza kusukumwa.Pasipo hata ya
kunisemesha wakaanza kunisukuma na kunipeleka nisipo pajua huku nyuso
zao zikiwa na tabasamu ambalo sikuliewewa nini maana yeke
ITAENDELEA...