
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amezindua
kiwanda cha kuunganisha matrekta cha Ursus na kiwanda cha Nondo cha
Kiluwa ambapo amewataka wawekezaji kujitokeza kwa wingi kwani Serikali
iko nao bega kwa bega.
"Kiwanda
ni kikubwa na kinatoa nondo ambazo zinaweza kujenga daraja lolote
Tanzania au Ulaya.Tanzania tuna chuma, kwa nini tuagize chuma kutoka
Brazil au China.
"Wawekezaji
watafute njia ya kutumia chuma cha Tanzania badala ya kuagiza nje ya
nchi na nashauri Ajira zianze kwanza kwa vijana wa Mkoa wa Pwani'',
amesema Rais Dkt. Magufuli na kuongeza kuwa serikali inampango wa
kujenga barabara kubwa ya lami ya njia sita kutoka Dar mpaka Chalinze
ambapo amewataka watanzania kuvilinda viwanda na amani ya Tanzania

0 comments:
Chapisha Maoni