Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘TAKUKURU’ leo August 3, 2017
imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Mmiliki wa Kampuni ya
kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi hatotibiwa nje ya nchi wala
Hospitali ya Muhimbili, bali atatibiwa Hospitali ya Amana na Lugalo.
Mwendesha
Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma
Shaidi kuwa Sethi hana sifa ya kutibiwa nje ya nchi wala Hospitali ya
Taifa Muhimbili, bali ni Amana na Lugalo ambapo kuna ulinzi na usalama.
Aidha,
Swai ambaye amedai watampeleka Sethi Hospitali ndani ya siku 14,
ameyaeleza hayo baada ya Wakili wa utetezi, Alex Balomi kudai kwamba
hadi sasa Sethi hajapewa matibabu licha ya Mahakama kuamuru atibiwe.
Kutokana
na hatua hiyo, Hakimu Shaidi alisema hakutoa amri ya Sethi kutibiwa nje
ya nchi, bali alitoa amri ya kutibiwa ikiwezekana Muhimbili, hivyo
ameutaka upande wa mashtaka kuhakikisha ndani ya siku 14 mshtakiwa
anapatiwa matibabu ambapo kesi imeahirishwa hadi August 17, 2017.
0 comments:
Chapisha Maoni