Serikali
imeombwa kukomesha kampeni mbalimbali zinazoanzishwa ikiwamo ya 'Baki
Magufuli' ili kuondoa sintofahamu iliyopo kwamba wenye kampeni hizo
wanatumwa na Rais John Magufuli.
Hayo
yamesemwa leo Alhamisi Agosti 3 na Shirika Lisilo la Kiserikali la
Vijana na Wanawake (Tafeyoco) wakati wakizungumza na wanahabari kuhusu
hali ya utawala bora na demokrasia inayoendelea nchini.
Mwenyekiti
wa Tafeyoco, Elvice Makumbo amesema kampeni hizo siyo muda wake kwa
sasa kwani zinatachochea kuzalisha kwa kampeni nyingine hali itakayoleta
mvurugano nchini.
"Tukiwaacha
hawa wenye kampeni ya 'Baki Magufuli' watazaliwa wengine wenye kampeni
ya 'Ondoa Magufuli' madarakani na wao watataka kuisambaza kampeni yao," amesema Makumbo.
Makumbo
amesema ni wakati muafaka kwa Serikali kupiga marufuku kampeni hizo,
kwani Tanzania inaongozwa kwa Katiba inayoeleza awamu ya kwanza ya rais
ni vipindi vitano baada ya hapo uchaguzi mkuu mwingine unaitishwa.
Amesema
Rais Magufuli anafanya kazi kubwa kuiongoza nchi na kwamba haitaji
‘tochi’ kupima uwezo wake hivyo kuanzisha kampeni za yeye kubaki ni
kutengeneza chuki kati yake na Watanzania ambao wanaikubali kazi yake.
Mbali
na hilo, Makumbo amewataka viongozi wa vyama siasa nchini kuacha tabia
ya kuwatumia vijana kuendeleza siasa katika mitandao ya kijamii, kwani
baadhi ya vijana wanatumia nafasi hiyo kuandika habari za uchochezi
dhidi ya Serikali.
0 comments:
Chapisha Maoni