Mwalimu
wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Igurubi, Maganga Ngassa (35)
amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga kwa tuhuma ya kufanya
mapenzi na mwanafunzi wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari kidato
cha nne, Kata ya Mwisi wilayani hapa.
Mwendesha
Mashitaka wa Polisi Igunga, Elimajid Kweyamba alidai mbele ya Hakimu
Juhudi Mdonya, kwamba Julai 25, mwaka huu saa 9 alasiri katika nyumba ya
kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Forest au Chacha iliyoko Mtaa wa
Mwayunge mjini Igunga, kinyume na sheria za nchi, Ngassa alifanya
mapenzi na mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 anayesoma shule ya
sekondari iliyoko Kata ya Mwisi kidato cha nne (jina linahifadhiwa).
Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 18, mwaka huu itakapotajwa tena.
0 comments:
Chapisha Maoni