Chama
cha CUF kimedai kuwa, licha ya uwepo wa hujuma zinazofanywa na baadhi
ya watu ili kumuondoa madarakani Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif
Shariff Hamad, katibu huyo ataendelea kubaki kwenye nyadhifa yake hadi
pale Mkutano Mkuu halali wa CUF utakapotengua ukatibu mkuu wake.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Agosti 5, 2017 jijini Dar es Salaam, Kaimu
Naibu Katibu Mkuu CUF, Joran Bashange alidai kuwa baadhi ya taasisi za
serikali zinafanya hujuma ya kutotambua maamuzi ya Maalim Seif kwa lengo
kumfanya Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na maamuzi yake kutambulika
kwenye taasisi hizo.
“Mpaka
tone la damu la mwisho linatokea, Katibu Mkuu ataendelea kubaki katibu
hadi pale mkutano mkuu wa chama utakapobadilisha maamuzi hayo. Taasisi
hizo hazimtambui kwa maneno lakini kisheria zinamtambua hata mahakama
zinamtambua Maalim Seif kuwa Katibu Mkuu wa CUF,” alisema na kuongeza.
“Maamuzi
yote anayofanya Lipumba yanaratibiwa, ili kuiondoa CUF. Seif ametuma
barua nyingi za kusimamisha uanachama baadhi ya watu lakini Ofisi ya
Msajili haitaki kuzifanyia maamuzi.”
Bashange alidai kuwa, Maalim Seif ataendelea kutekeleza majukumu yake.
0 comments:
Chapisha Maoni