Watu
watatu wakiwamo watoto wadogo wawili wamekufa huku wawili wakinusurika
baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama kwenye mto Ruvu,
walipokuwa wakijaribu kuvuka kutoka Vigwaza kwenda Mlandizi mkoani
Pwani.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Jonathan Shana
alisema licha ya watu hao kubainika kufa, nahodha wa mtumbwi huo
hajulikani alipo. Shana alisema ajali hiyo imetokea Jumamosi saa 4:00
asubuhi kwenye mto Ruvu wilaya ya kipolisi Chalinze.
“Ajali
hiyo imepoteza maisha ya watoto wawili ambao ni Nusrat Haji miezi minne
na Feisal Hamza mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu pamoja na Sikuzani
Musa (41), ambaye mwili wake bado haujapatikana,” alisema Kamanda Shana.
Kamanda
Shana aliwataja walionusurika ni Zuwena Ramadhan (29) na Tero Mziray
(20) ambapo dereva wa mtumbwi huo hajulikani alipo na inaaminika hakufa
maji.
“Chanzo
cha mtumbwi huo kuzama bado kinachunguzwa na miili ya marehemu
imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi,” aliongeza.
Aliwataka
wamiliki wa vyombo hivyo kuhakikisha vinakuwa kwenye hali nzuri ili
kuepukana na ajali kama hizo ambazo zinapoteza uhai wa watu kutokana na
ubovu.
0 comments:
Chapisha Maoni