Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Kenya zimefanya
mazungumzo ya pamoja na kutatua vikwazo vilivyokuwa vikiikabili sekta
ya biashara baina ya nchi hizo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga
alitoa taarifa juu ya kumalizika kwa tofauti za kibiashara baina ya nchi
hizo.
“Bidhaa
za Tanzania zilizowekewa vikwazo na nchi ya Kenya ni unga wa ngano
pamoja na gesi ya kupikia (LPG). Aidha juhudi, za Serikali ya Tanzania
kuona vikwazo hivyo vinaondolewa na Serikali ya Kenya kwa wakati
hazikuzaa matunda, hivyo Serikali ya Tanzania nayo iliweka vikwazo kwa
bidhaa za maziwa na sigara kutoka Kenya kuingia katika soko la
Tanzania,” alifafanua Dkt. Mahiga.
Alisema
kuwa kutokana na mahusiano mazuri ya udugu yaliyopo kati ya Tanzania na
Kenya na kwa kujali manufaa mapana ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru
Kenyatta na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli walikubaliana kuzungumza na kutoa vikwazo vya biashara hizo.
Aidha,
Dkt. Mahiga amesema, nchi hizo zimekubaliana kuunda Tume ya pamoja
ambayo itakuwa na jukumu la kuepusha tofauti za kibiashara kati ya
Tanzania na Kenya pamoja na kutolea ufumbuzi changamoto za kibiashara
kati ya nchi hizo mbili pindi zinapojitokeza.
Tume
hiyo itaongozwa na Mawaziri wa mambo ya Nje wa Tanzania na Kenya na
kujumuisha mawaziri wanaohusika na masuala ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Biashara, Fedha, Mambo ya Ndani ya Nchi, Kilimo, Uchukuzi na
Utalii wa nchi hizo.
0 comments:
Chapisha Maoni