Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana alisomewa mashtaka ya uchochezi
na kurudishwa rumande akisubiri hatma ya dhamana yake.
Lissu alisomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbert Mashauri.
Mawakili
watano wa upande wa Jamhuri waloshiriki katika kesi hiyo, waliiambia
Mahakama kuwa Lissu alitenda kosa hilo la jinai Julai 17 mwaka huu
katika eneo la Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Lissu
ambaye alikuwa akitetewa na jopo la mawakili 20 wakiongozwa na Fatma
Karume, alikana mashtaka dhidi yake. Mbunge huyo pia alisikika akisema,
“kwakweli halijawahi kuwa kosa la jinai.”
Baada
ya kusikiliza pande zote mbili Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi
Julai 27 ambapo hatma ya dhamana ya mwanasiasa huyo ambaye pia ni Rais
wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) itakapojulikana.
==>Hii ndpo hati ya shitaka lake
==>Hii ndpo hati ya shitaka lake
0 comments:
Chapisha Maoni