ILIPOISHIA
Wakiwa
katika hali bado ya kushangaa, madam Merya akaona gari mbili za polisi
zikisimama katika maegesho yaliyopo mbele yao. Wakashuka watu sita
kwenye gari mbili hizo. Kwa haraka madam Mery akamkumbatia Eddy na
kumgeuza upande mwengine na kuanza kumnyonya denda huku viganja vyake
vyote viwili vikiufunika uso wa Eddy na kuzidi kumnyonya denda Eddy
pasipio kumuhofia mtu wa aina yoyote. Shamsa akalishuhudia tukio hilo na
kumuonyesha Phidaya kitua anacho kifanya Madam Mery, jambo lililo
ipandisha hasira ya Phidaya mara dufu na kuanza kuwafwata madama Merry
na Eddy sehemu walipo simama.
ENDELEA
“Eddy hakikisha uwageukii wale askari”
Madam
Mery alizungumza kwa haraka kabla hata Phidaya ajawafikia. Kitendo cha
Phidaya kufika tu madam Mery akamuachia Eddy na kuingia kwenye gari
kuepusha mafarakano yasiyo ya lazima. Phidaya akataka kuingia kwenye
gari ili kumchomoa madam Mery ila Eddy akamuwahi na kumkumbatia na
kuanza kumnyonya mdomo, huku kwa pembe ya jicho akiwatazama askari hao
wanao elekea ndani ya lango la hospitali.
“Niachie”
Phidaya
alizungumza huku akijitoa mikononi m wa Eddy. Rahab, raisi Praygod na
Sa Yoo walibaki wakiwa na mshangao wasijue ni kitu gani ambacho
kinaendela kati ya watu hawa watatu.
“Tuondokeni, Phidaya ingia kwenye gari”
Eddy alizungumza kwa sauti nzito iliyo onyesha msisitizo, taratibu Phidaya akajikuta akiingia kwenye gari hiyo.
“Itabidi kupakatana hapa, siti hazitoshi”
Rahab
alizungumza huku akifungua mlango wa mbele, raisi Praygod naye akaingia
siti ya mbele, ikabidi Eddy akae katikati ya madam Mery na Phidaya,
huku Shamsa akipakwa na Phidaya na Sa Yoo akipakatwa na madam Mery.
Wakaondoka eneo hilo la hospitalini pasipo askari walio kuja kuwatafuta
kuwaona.
***
Yassin na vijana wake wakaonye vitambulisho kwa askari walio eneo hilo.
Kutoka vitambulisho havina utofauti kabisa na vitambulisho na askari
halali, hapakuwa na mtu aliye weza kuwatilia mashaka hata kidogo.
“Tunahitaji kuzungumza na daktari wa zamu”
Yassin alimuambia mmoja wa nesi, aliye kaa sehemu ya mapokezi
“Ngoja niwasiliane naye”
Nesi
huyo akanyanyua mkonga wa simu na kumpigia daktari wa zamu na kumuomba
aweze kufika sehemu ya mapokezi kuja kuafanya mahojiano na askakari hao.
Hazikupita dakika tano daktari wa zamu akafika eneo hilo la mapokezi,
akasilimiana na Yassin ambaye hadi sasa hivi hakuna mtu hata mmoja
ambaye ameweza kumgundua kwamba yeye ndio gaidi aliye fanya uvamizi
masaa kadhaa nyuma.
“Kuna mtu tunahitaji kumuhoji maswali mawali matatu na amelazwa hospitalini hapa”
“Ingekuwa ni vizuri kama ukanieleze jina la mtu huyo anaitwa nani ili tuweze kutazama kwenye vitabu vyetu vya kumbukumbu”
Yassin
akatoa simu yake mfukoni na kumuonyesha daktari huyo picha ya Eddy,
aliyo itazama kwa muda mchachwe na kuweza kumkumbuka mtu aliye weza
kumpatia huduma ya kwanza aliye sadikika kwamba alivamiwa na gaidi.
“Huyu yupo wodini, nilimuhudumia baada ya tukio la uvamizi kutoa”
“Tunakuomba utupeleke kwenye chumba chake”
“Ila kuna usalama kweli?”
“Usalama upo, dokta mbona una wasiwasi”
“Ahaaa haaa hamna”
Daktari
alijing’ata ng’ata huku akijaribu kuvuta kumbukumbu ya sura ya Yassin,
aliye anza kumtilia mashaka ila kofia aliyo ivaa Yassin kidogo iliweza
kumpa matumaini daktari huyo na kujiamini kwamba labda mtu huyo atakuwa
sio yeye. Wakafika kwenye wodi ambayo Eddy alilazwa, kila mtu alibaki
akishangaa hata daktari mwenyewe.
“Amekwenda wapi huyu mtu?”
Daktari alijiuliza huku akipiga hatua kueleka chooni, akafungua mlango na kukuta hakuna mtu yoyote
“Bosi kwani amevaaje vaaje mtu huyo?”
Khalid alimuuliza Yassin huku akimtazama machoni. Yassin akavuta picha ya jinsi Eddy alivyo valiaa.
“Amevaa shati jeusi, lina mistari mistari myeusi kwenye mikono”
“Shiti
bosi, mbona kama huyo mtu nilimuona kwenye maegesho ya magari muda ule
tulivyo fika, ila alitupa mgongo na alikuwa akipigana kisi na mkewe
sijui”
“Nini?”
“Ndio bosi ninauhakika, kama ni mtu aliye valia shati yeusi basi ninauhakika ndio huyo niliye muona”
“Asante dokta”
Yassin
kwa haraka akatoka nje akiwa na vijana wake, wakaingia kwenye magari,
wakaondoka eneo la hospitali. Walipo fika getini Yassin akamuamuru
kijana wake asimamishe gari ili kumuuliza mlinzi wa getini. Akamuelezea
jinsi muonekanano wa Eddy na akamuonyesha picha mlinzi huyo.
“Sijamuona kabisa”
“Je kuna gari lolote lililo toka eneo hili dakika chache?”
“Magari yaliyo toka yapo kama kumi na kila moja limeelekea upande tofauti wa barabara”
“Asante. Ednesha gari”
Yassin
alizungumza huku akifunga kioo cha gari na kuondoka eneo la hospitali
matumaini ya kumpata Eddy yakiwa yamemuishia kabisa. Hakujua afanye nini
ili kumpata kwa maana jiji la Cairo ni kubwa sana na ni ngumu kumtafuta
mtu mmoja tu.
***
Breki ya kwanza ikawa nyumbani kwa raisi Praygod. Wakashuka kwenye gari
kila mmoja akiwa amechoka sana huku matumbo yao yakisumbuliwa na njaa
waliyo dumu nayo kwa muda mrefu sana. Sa Yoo moja kwa moja akaelee
lilipo friji akafungua na kutoa chupa ya soda na kuanza kuigugumia, bila
ya mapumziko.
“Mmmm best utapaliwa”
Shamsa alizungumza huku akitabasamu
“Mmmm
bora kupaliwa kuliko hii kiu niliyo kuwa nayo. Yaani tangu asubuhi
nilivyo ondoka hotelini sijakula chochote hadi muda huu”
“Ehee hivi ilikuwaje kuwaje hadi mukaja hospitalini?”
“Tulikuja kukuangalia, tulisikia kwamba uliwahishwa hospitalini na madam Mery baada ya wewe kuwa katika hali mbaya.”
“Tulivyo
ondoka asubuhi nilikuacha ulale kwa maana uliletwa umelewa chapachapa.
Sasa muda tunarudi hotelini tukaambia kwamba umewahishwa hospitalini,
kufika madam Mery anatuambia kwamba umefariki. Sasa muda ule ninakuona
pale mapokezi, niliingiwa na woga kiasi kwamba nikataka kuondoka. Ila
nilijikaza na kukufwata”
“Hapo sasa nimeanza kupata picha?”
“Picha gani?”
“Unajua
jana usiku kichwa kiliniuma sana, nikajisahau kama nimekunywa pombe.
Nilichukua zile dawa zako za kukuzuia maumivu ya kichwa, nikazinywa.
Kuanzia hapo sikuelewa nini kinacho endelea. Kuja kustuka najikuta nipo
mochwari”
“Mochwari…….??”
“Yaani wee acha tu, kunatisha kama nini na kuna ubaridi mkali”
“Jamani mabinti tusaidiane kupika”
Rahab
alizungumza na kuyakatisha mongezi ya Sa Yoo na Shamsa, hapakuwa na
aliye bisha, wakaingia jikoni na kuanza kusaidiana kupika.
“Mudabidi muweke tofauti zenu pembeni sasa”
Raisi Praygod alizungumza huku akiwa anawatazama Eddy, Phidaya na madam Mery alio kaa nao kwenye sebleni.
“Ila muheshimiwa haiwezekani, huyu malaya kumkisi mume wangu tena wa ndoa”
“Phidaya cha kumtusi mwenzio”
“Ahaaa kwa hiyo unamtetea huyo malaya, si ndio”
“Phidaya hembu kuwa na lugha ya busara. Tambua upo wapi na unazungumza na watu wa aina gani”
Raisi Praygod alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo na kumfanya Phidaya kukaa kimya, ila jazba yake bado inautawala moyo wake.
“Muheshimiwa ninaomba nizungumze kitu, ambacho kilinifanya mimi kuweza kufanya nilicho kifanya”
“Zungumza”
“Mimi
nilikuwa ni miongoni mwa wanachama wa D.F.E. Niliingia kwenye chama
hicho kutokana nilikuwa na musiano ya kimapenzi na Mzee Godwin ambaye
kwa sasa ni raisi wa Tanzania.”
Madam Mery alizungumza kwa sauti ya upole iliyo jaa unyeyekevu.
“Lengo
kubwa lilikuwa ni la kumteketeza Eddy ambaye ni mtoto wa mzee Godwin,
tena wa kumzaa naamini unalitambua hilo muheshiwa, kwamba Eddy huyo hapo
ni mtoto wa Godwin”
Raisi Praygod akatingisha kichwa akiashiria kwamba anatambua swala hilo.
“Ukiachilia
mbali swala zima la kumuua Eddy, ila D.F.E, inajishuhulisha na mambo
mengi duniani. Ni mtandoa mmoja wa siri ambao ni mkubwa na wenye nguvu
kulia hata kundi la Alquida. D.F.E inamatawi karibia dunia nzima. Na
ndio iliyo pelekea wewe kuangushwa kwenye uchaguzi kwa maana ndani ya
serikali yako kulikuwa na watu wa ngazi ya juu ambao walikuwa wakiungana
na Mzee Godwin.”
“Tukiachana
na hayo tuje kwenye wale askari tulio waona pale hospitalini. Naweza
kuwaambia kwamba hakuna askari pale. Yule jamaa mrefu anaitwa Yassin
alikuwa ni bodigadi wangu kipindi nipo kwenye mtandao wa D.F.E, ndio
maana niliweza kumtambua haraka sana nilipo weza kumuona pale kwenye
maegesho. Ninaimani walikuja kwa lengo la kumteka Eddy. Laiti wangemuona
sisi wote tungeangamia, kwa maana Yassin huwa ni mtu asiye na huruma
kwa mtu ambaye amekusudia kumuua"
Phidaya
akajikuta akishusha pumzi, kwa maana anamtambua vizuri mzee Godwin na
ndio mtu aliye sababisha yeye kuingia katika matatizo ya kupotezana na
mume wake.
“Tupo katika hali ya hatari, tunatakiwa kuwa tayari kwa lolote muda wowote kuanzia sasa.”
“Sasa tutafanyaje jamani?”
Raisi Praygod alizungumza kwa unyonge akionyesha hivi hivi ni dhaifu katika swala hilo.
“Muheshimiwa
naomba hiyo kazi uniachie mimi, ninaimani kwamba kila jambo litakwenda
sawa. Nitahakikisha kwamba ninamuu mzee Godwin”
“Honey sio kiurahisi kama unavyo hisi. Wewe mwenyewe unamjua baba yako alivyo na roho mbaya”
“Hakuna mtu mwengine anaye weza kupambana na mzee Godwin zaidi yangu. Inabidi tufanye mpango wa kurudi Tanzania”
“Eheeee Tanzania!!?”
“Ndio
honye ni lazima turudi Tanzania, kule ndio kwetu. Nilazima kuitetea
nchi yangu kwa maana kwa sasa wananchi wanapitia kwenye kipindi kigumu
sana”
“Baby mimi sirudi nitakaa hapa hapa?”
Phidaya
alizungumza kwa woga mkubwa sana. Sa Yoo akaingia sebleni na kuwatazama
watu wote kwa haraka akagundua kuna jambo ambalo linaendelea eneo hilo
“Jamani munaombwa muje mezani chakula kimesha ivaa”
“Sawa tunakuja”
Raisi
Praygod alijibu, Sa Yoo akaondoka na kuacha ukimya ukitawala. Hapakuwa
na mtu aliye zungumza jambo lolote. Madam Mery akanyanyuka na kueleka
kwenye meza na kuwaacha Phidaya, Eddy na raisi Praygod.
“Jamani natangulia mezani”
Raisi Praygod aakanyanyuka na kuondoka. Eddy akamtazama Phidaya usoni
“Mke wangu tunabidi kurudi Tanzania. Nahitaji kukulinda siwezi kukuacha ukae mbali nami?”
“Ila honey naogopa”
“Usiogope nitakulinda hadi mwisho wa maisha yangu”
Eddy alizungumza huku taratibu akimvuta Phidaya kifuani mwake na kumkumbatia.
“Nakupenda sana Eddy wangu”
“Nakupenda pia mke wangu. Haya twende tukale”
Wote
wawili wakanyanyuaka na kuelekea kwenye meza ya kulia, wakawakuta watu
wote wakiwa amesha jitengea chakula. Kila mtu akaka kwenye kiti chake na
kuendelea kula huku mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea.
“Jamani, inatubidi kuanza kupanga mipango ya kurudi Tanzania. Ila tutambue kwamba Tanzania tunakwenda kwa kazi moja tu”
Eddy alizungumza huku akimtazama kila mmoja, kwa umakini.
“Kazi gani?”
Sa Yoo aliuliza huku akirudisha kwenye sahani yake, kijiko kilicho jaa wali.
“Kazi ya kumuangusha raisi Godwin, na kumtoa madarakani”
“Kumuangusha raisi. Si kazi kubwa hiyo?”
“Ndio
ni kubwa Sa Yoo. Ila ni lazima kuweza kumuangusha, kuanzia kesho
asubuhi tutaanza kupeana majukumu ya nini kufanya tukifika nchini
Tanzania”
“Sawa”
Wakamaliza
kula, kutoka na uchovu hapakuwa na mtu aliye hitaji kupiga stori, Rahab
akamuonyesha kila mtu chumba chake. Eddy na Phidaya ikawa ni usiku wao
wa kufanya starehe ambayo kwa miaka mingi waliipoteza. Shamsa kila
alivyo jigeuza kitandani, usingizi haukumjia.
Akamtazama
Sa Yoo anee endelea kukoroma na usingizi mzito alio kuwa nao. Taratibu
Shamsa akashuka kitandani, akavaa nguo ya kulalia aliyo pewa na Rahab.
Alipo
hakikisha kwamba amejifunga vizuri akatoka chumbani kwa lengo la kwenda
sebleni kutazama japo filamu. Katika kukatiza katika chumba alicho lala
Phidaya na Eddy, akasikia miguno ya mapenzi anayo itoa Phidaya,
akionekana kufurahia sana kwa penzi analo pewa na mumewe.
Shamsa
akajikuta mwili mzima ukisisimka, chuchu zikamsimama, mapigo ya moyo
yakaanza kumuenda mbio. Jasho la shingo likaanza kumwagika taratibu.
Akataka kupiga hatua kuondoka, ila miguu iliingiwa na uzito ambao
hakujua hata umetokea wapi. Roho moja ikawa inamshauri kuchungulia
kupitia tundu la kitasa cha mlangoni, huku roho moja ikimshauri kuondoka
eneo hilo la mlangoni. Taratibu Shamsa akajikuta akiinama na
kuchungulia kwenye tundu hilo la kitasa, kwa bahati nzuri hapakuwa na
fungua, ikawa ni rahisi kwa yeye kuweza kuona ndani.
Akamshuhudia
jinsi Phidaya anavyo katika huku akiwa amemkalia Eddy mapajani, Shamsa
akameza fumba zito la mate huku akizidi kukaza jinsi kumshuhudia Phidaya
anavyo onyesha ufundi wake juu ya kiuno cha Eddy. Taratibu Shamsa
akashika kitasa cha mlango huo, kwa uzuri zaidi akakuta mlango
haujafungwa. Taratibu akausukuma, akachungulia na kugundua hakuna aliye
muona katia ya Eddy na Phidaya.
Akazazama ndani na kuurudishia mlango taratibu, kwa jinsi Phidaya na
Eddy walivyo zama kwenye dibwi la mahaba, wakazidi kumchanganya Shamsa,
aliye jikuta akianza kujipapasa kuanzia kwenye maziwa na kushuka chini.
Mzuka wa kufanya mapenzi, akaingiza kiganja chake kwenye bikini aliyo
ivaa na kuanza kullisugua sugua tunda lake, kila jinsi Phidaya alivyo
zidi kukatika ndivyo jinsi Shamsa alivyo zidi kuongeza kasi ya kusugua
tunda lake ambalo hadi wakati huu hakuna mwanaume aliye weza kulionja.
Kwa mzuka mkali wa mapnezi, Shamsa akajikuta akiegemea ukutani, na
kuandelea kujichua. Kinguo cha usiku alicho kivaa akaona kinamsubua
katika shuhuli yake hiyo.
Akakivua
na kukitupia pembeni, akamalizia na chupi akabakiwa kama alivyo zaliwa
na kuendela kujichua uku akigugumia kwa raha anayo ipata. Katika kusogea
sogea huku akiwa ameuegemea ukuta kwa bahati mbaya akaegemea swichi, na
gafla taa ya chumba hicho ikawaka na kuwastua Eddy na Phidaya ambao
wote macho yao wakayatupa mlangoni na kumkuta Shamsa akimalizia kufika
kileleni kwa safari yake nzima ya kulichua tunda lake.
SORRY MADAM (77) (Destination of my enemies)
Shamsa akashusha pumzi nyingi, huku taratibu akiyafumbua macho yake.
Kwa mshangao walio upata Phidaya na Eddy, ukamfanya Shamsa akibaki
akitabasamu asijue ni nini cha kufanya.
“Vipi?”
Eddy
aliuliza huku akiwa amakazia macho ya hasira Shamsa. Shamsa hakujibu
kitu cha aina yoyote zaidi ya kubaki akiwa anaweweseka. Eddy akataka
kunyanyuka kitandani ila Phidaya akamzuia.
“Unataka kwenda wapi wakati huna hata nguo?”
“Jamani samahani”
Shamsa
baada ya kugundua dhairi kwamba Eddy amekasirika, akafungua mlango
akatoka. Kwa haraka Phidaya akashuka kitandani na kuzima taa. Mwanga wa
mbaramwezi unao ingia kupitia dirishani, unakifanya kila kitu kilichomo
ndani ya chumba kuoneka vizuri.
“Hembu kaa na mwaoa na umfunzee, hii tabia aliyo ionyesha sijaipenda”
Eddy
alizungumza kwa hasira kiasi kwamba Phidaya akaka kimya kwa maana
anamtambua mumewe vizuri na huwa akizungumza kitu huwa ana maanisha
katika hilo. Hata hamu ya kuendela na tendo hilo Eddy hakuwa nalo
akajifunika vizuri shuka na kugeukia upande wa pili na kumpa Phidaya
mgongo.
Mapigo ya moyo yakazidi kumuenda mbio Shamsa, hakujua ni kitu gani
kinaweza kutokea asubuhi pale atakapo onana na Eddy apmoja na Phidaya.
Kitu kingine kilicho mchanganya akili ni kuhusiana na nguo zake alizo
ziacha katika chumba cha Eddy na Phidaya.
‘Eeheeee Mungu wangu kwa nini mimi?’
Shamsa
alizidi kujiuliza huku akiwa amelala chali kitandani, Sa Yoo hakujua
kinacho endelea zaidi ya kuendela kuponda usingizi kutokana na kuchoka
sana kwa mizunguko mingi ya kutwa nzima.
Asubuhi
na mapema, Shamsa akawa mtu wa kwanza kuamka kitandani, akaingia bafuni
na kuoga, kisha akavaa nguo zake. Kwa haraka akeleeka jikoni. Bila ya
kufwata maelekezo ya mama mwenye nyumba Rahab. Akaanza kuandaa kifungua
kinywa cha watu wote. Baada ya kuhakikisha ametengeneza vifungua kinywa
cha uhakika, akaviweka mezani tayari na kuanza kuwasubiria wezake
kuamka.
Majira ya saa moja asubuhi tayari kila mmoja alisha amka na kukuta kifungua kinywa tayari jambo lililo mfurahisha sana Rahab.
“Umetengeneza kifungua kinywa ambacho ninakipenda”
“Kweli madam Rahab?”
“Kweli, huwa napenda sana mayai na soseji, ndio maana nimeyajaza kweye friji”
“Karibu mezani”
Shamsa
alizungumza kwa furaha, kiasi kwamba hata Sa Yoo mwenyewe akamshangaa.
Kwa jicho kali alilo tazamwa na Eddy, furaha ya Shamsa ikatoweka usoni
mwake. Wakajipatia kifungua kinywa baada ya kumaliza, mipango ya kurudi
Tanzania ikaanza kupangwa. Kila mmoja akaanza kukabidhiwa jukumu lake na
Eddy ambaye ndio kiongozi wa mpango mzima.
Baada
ya kila mmoja kupatiwa jukumu alilo limudu, mpango wa Eddy kutafutiwa
daktari wa kuibadilisha sura yake na kufanyiwa oparesheni nyingine,
ukaanza. Haikuchukua mud asana raisi Praygod akampata daktari Bi
Jaquline Annel. Daktari bingwa wa kutengeneza sura za bandia, anaye
tokea nchini Marekani kwa bahati nzuri Bi Jaquline Annel, yupo nchini
Misri kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.
“Nitakuja
hapo kutokana na heshima yako muheshimiwa raisi, kwa maana hiyo kazi
ambayo unayo taka kunipa ipo nje ya ratiba yangu kwa maana nipo
mapumzikoni”
Sauti ya dokta Bi Jaquline Annel, ilisikia kwenye simu ya raisi Praygod.
“Nitashukuru ila nipo tayari kwa kukulia kiasi chochote cha pesa utakacho kihitaji”
“Ok nipatie nusu saa nitakuwa nimesha fika hapo nyumbani kwako, kwa msaada wa dereva wangu”
“Sawa daktari”
Raisi
Praygoda akakata simu na kumgeukia Eddy aliye kaa nyuma yake akiwa na
hamu ya kutaka kufahamu ni jibu gani ambalo raisi Praygod anaweza
kulipata.
“Tumshukuru Mungu, amekubali, ameniambia ndani ya nusu saa atakuwa hapa.”
“Ohoo
asante sana muheshimiwa raisi naamini kazi iliyopo mbele yangu
haitakuwa ngumu kama nitakavyo ifanya nikiwa katika sura yangu ya
kawaida”
“Usijali nipo kwa ajili yako kwa sasa”
Kama alivyo ahidi dokta Bi Jaquline Annel, ndani ya nusu saa simu ya
raisi Praygod ikaanza kuita, kwa haraka akaipokea na kuiweka sikioni.
“Nipo nje ya geti la nyumba yako namba 2215”
“Sawa ninakuja”
Raisi
Praygod akatoka nje ya nyumba yake na kumkuta dokta Jaquline Annel
akiwa ndani ya gari lake. Raisi Praygod akafungua geti na gari likaingia
kisha akalifunga.
“Karibu sana dokta Jaquline”
“Asante, aisee unaanza kuzeeka kwa sasa?”
“Kweli ni miaka mingi hatujaona”
“Mizunguko mingi sana kiongozi ni miaka kama ishirini hivi eheee?”
“Ndio mara ya mwisho, tulionana nikiwa waziri wa mambo ya nje Tanzania”
“Kweli,
nakumbuka kipindi kile ulikuja chuoni kuwatembelea watanzania,
nakumbuka nilikuwa na rafiki yangu mtanzania ambaye alinifundisha
kiswalihi kabisa hadi ile siku ninasoma risala ya Kiswahili mbele yako
watu wote hawakuamini”
Bi.
Jaquline Annel ni mzungumzaji sana, urefu wa mwili wake na wembamba
wake, dhairi uliweza kumfanya kuwa mchangamfu kwa watu anao fahamiana
nao. Akakaribishwa ndani na kuwakuta watu wote wakiwa wamekaa sebleni.
“Karibu sana”
Dokta
Bi Jaqulne Annel akasalimiana na kila mtu, kisha akaka kwenye sofa
ambalo aliendaliwa kukaa. Raisi Praygod akaanza kuzungumza dhamira iliyo
mfanya dokta Bi Jaquline Annel kuweza kufika hapo. Akamuonyesha Eddy
ambaye ndio muhusika mkuu wa kuweza kufanyiwa utengenezaji wa sura hiyo.
“Mmmmmm, ngoja kabla hujaendelea na mazungumzo muheshimiwa raisi. Je munataka sura ambayo atadumu nayo kwa muda mrefu au mfupi?”
“Muda mrefu kwa maana naamini umesikia sikia habari za nchi yangu ya Tanzania kwa sasa zinavyo kwenda?”
“Yaaa nimesikia, na ndio maana leo ulivyo nipigia simu nikashangaa sana.”
“Basi
hapa wote unao waona wapo katika mpango wa ukombozi wa mamilioni ya
Watanzania kwa sasa wanaumia na kutesaka na uongozi uliopo”
Raisi
Praygod alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Kila mmoja alikaa
kimya akiwa anamsikiliza kwa umakini, ikamuonyesha ni jinsi gani hali
hiyo inamuuzunisha na kumuumiza kila mmoja, hata dokta Bi Jaquline Annel
alilengwa lengwa na machozi.
“Nitawasaidia, nilipanga kuwalipisha kiasi kama ninacho walipisha watu wengine, ila nitawafanyia kwa upendo na amani”
“Nashukuru sana dokta”
Eddy
alizungumza kwa sauti ya unyenyekevu. Dokta Bi Jaquline Annel akatoa
maelekezo ya siku ambayo atamfanyia Eddy oparesheni hiyo katika nyumba
hiyo hiyo ya raisi Praygod.
“Itabidi leo niondoke na ndege ya kukodi nirudi New York, kesho kutwa nitakuwa hapa na kazi itaanza rasmi”
“Sawa dokta”
Wakapata
chakula cha mchana kwa pamoja na dokta Bi Jaquline Annel akaeleka
hotelini, huku akiwa tayari amesha weka oda ya ndege ya kukodi.
Akausanya kila kilicho chake na kuelekea uwanja wa ndege na kuanza
safari ya kurudi Marekani.
***
Ahadi ya dokta Bi Jaquline Annel, ikakamilika, ndnai ya siku tatu akawa
tayari amesha rejea Misri na moja kwa moja akaelekea nyumbani kwa raisi
Praygod mara baada tu ya kutoka uwanja wa ndege. Akapokelea kwa furaha
kubwa, huku chumba ambacho aliomba kiweze kutengwa kwa ajili ya kazi
hiyo kilisha andaliwa.
Zoezi
la kwanza likaanza, akanpiga Eddy picha karibia ishirini za uso wake,
akaziingiza kwenye laptop yake anayo fanyia kazi. Akaanza kuunda sura
ambazao zingeendana na sura ya Eddy. Alipo hakikisha ametengeneza sura
nne kwenye laptop yake, akamuita Eddy na raisi Praygod kuweza kuchagua
ni sura gani ambayo Eddy angeweza kuipenda.
“Hii itakuwa ni nzuri kwangu”
“Itakufanya uonekane mzuri zaidi ya hapo”
Dokta Bi Jaquline Annel alitania kidogo na kuwafanya Eddy na raisi Praygod kucheka kidogo
“Ndio vizuri asijulikane kabisa”
“Haya mimi nafanya mutakavyo, hii sura ninayo kuwekea, itachukua hata miaka mitatu bila kutoka”
“Kweli dokta?”
“Ndio
Eddy, na hakuna mtu atakaye weza kujua ni sura ya bandia kwa mana
utaalamu ninao utumia ndio umenifanya niwe na mafanikio makubwa sana,
muulize hata raisi wako hapa. Ananijua”
Dokta
Bi Jaquline Annel hakusita kuweza kujielezea ubora wa kazi yake ambayo
kwa sasa ni mwaka wa kumi na nane anaifanya na imemuingizia pesa nyingi
na ameifanya kwa watu wengi maarufu duniani hata magaidi ambao dunia
inapata shida katika kuwatafuta, ila aliweza kuwafanyia bila woga,
alicho kijali kwake ni malipo yake tu. Usiri wa kazi yake hiyo ulizidi
kumuongezea idadi kubwa ya wateja ambao alihitaji kubadilishwa sura.
Baada ya doka Bi Jaquline Annel kufanya kazi ya kuitengeneza sura aliyo
ichangua Eddy kwa vifaa vyake maalumu. Kazi ikaanza usiku.
Bi
Jaquline Annel akawaomba watu wote kuto kuingia kwenye chumba hicho kwa
maana kazi yake anaifanya kwa utulivu mkubwa na haitaji kabisa mtu
kuweza kuona ni nini anacho kifanya. Kila mmoja aliweza kutii, japo
Phidaya alikuwa na mashaka kidogo, ila Sa Yoo aliweza kumfariji. Haidi
inafika majira ya saa kumi alifajiri, dokta Bi Jaquline Annel, tayari
alisha maliza kazi, japo uso mzima wa Eddy aliufunga na bandeji, huku
sehemu ya pua akiacha vitundu viwili vinavyo weza kuingiza hewa.
“Hujalala hadi sasa hivi?”
Dokta Bi Jaquline Annel alimuuliza Phidaya aliye mkuta amekaa sebleni akitazama Tv huku watu wengine wakiwa wamelala.
“Vipi kazi imeenda vizuri dokta?”
Phidya hakujibu swali alilo ulizwa zaidi ya yeye kuuliza swali.
“Ndio usijali, bandeji hiyo nitaitoa baada ya masaa ishirini na tano”
“Sijakuelewa dokta?”
“Usinyanyuke, hembu kaa tuu kwenye sofa.”
Dokta Bi Jaquline Annel alizungumza huku na yeye akikaa kwenye sofa. Akamtazama Phidaya usoni akagundua wasiwasi alio nao.
“Eddy ni nani kwako?”
“Ni mume wangu wa ndoa”
“Ahaaa hongera sana. Una mume mzuri sana”
“Asante”
“Akipona utamsahau, kwa mana atakuwa ni bonge la handsome, sasa angalia visichana visichana visije vikakupora”
“Hahahaa hakuna dokta”
Wakaendelea
na mazungumzo ya hapa na pale hadi wote wakaipitiwa na usingizi. Masaa
yakazidi kwenda na kukatika. Baada ya masaa ishirini na tano. Dokta Bi
Jaquline Annel akafungua bandeji alizo mfunga Eddy uso mzima.
“Pole kwa kukulaza kwa muda mrefu”
“Asante dokta”
“Naaamini njaa ndio inayo kusumbua. Ila kabla hujanyanyuka chukua hichi kioo ujitazame”
Dokta
Bi Jaquline Annel akampatia Eddy kioo, taratibu akakisogeza mbele ya
sura yake. Eddy akabaki akiwa ameufumbua mdomo wake kwa mshangao.
Hakuamini kama ni yeye, sura yake imebadilika kwa asilimia kubwa tena
kiasi cha kujikuta akianza kucheka mwenye huku tabasamu pana likiwa
limetawala usoni mwake.
“Unaweza sasa kunaynyuka na kwenda sebleni”
Eddy
akanaynyuka taratibu, kitu kilicho msaidia kukaa kwa masaa yote hayo
pasipo kuingiza kitu chochote mdomoni, ni mazozi na uvumilivu alio
pitia kwenye maisha yake. Eddy akatoka na kufika sebleni na kuwakuta
watu wote wakiwa wameka wakitazama Tv.
“Haloooooo”
Watu wote wakageuka, na kumtazama Eddy. Kila mmoja akajikuta akishangaa kumuona Eddy katika sura hiyo.
“Ni wewe?”
Rahab alizungumza huku akiachia tabasamu pana.
“Ni mimi, nimekuwaje?”
“Umebadilika umekuwa so so handsome”
Phidaya
akasimama na kumkumbatia Eddy. Wakamuandalia chakula Eddy, aliye kila
kwa kasi kutokana na njaa inayo ikwangua utumbo wake. Baada ya kumaliza
kula akaingia bafuni na kuoga.
“Jamani nimemaliza kazi yangu”
Dokta
Bi Jaquline Annel alizungumza huku akimtazama raisi Praygod usoni.
Raisi Praygod aratibu akasimam na kumpa mkono wa shukrani Bi Jaquline
Annel.
“Nakuahidi nikirudi madarakani nitahakikisha ninakupa zawadi ambayo huto isahau kwenye maisha yako”
“Ni wewe tu”
Kila
mmoja akamshukuru doka Bi Jaquline Annel wakafanya sherehe ndogo ya
kuagana naya kisha bi Jaquline Annel akarudi hotelini kuendelea na
mapumziko yake ya mwisho wa mwake. Harakati za kutafuta hati ya
kusafiria kwa upande wa Eddy ikaanza, hapakuwa na kipingamizi kikubwa
kutona na kutumia pesa. Baada ya hati ya kusafiria ya Eddy kupatikana
ikiwa na jina la Erickson Forrd. Safari ya kueleka nchini Tanzani
ikaanza.
***
Picha
ya Eddy ilitandazwa kwa wafanyakazi wachache wa uwanja wa ndege wa
mwalimu J.K Nyerere ulipo Dar es Salaam nchini Tanzania. Kila mfanyakazi
aliye weza kupewa picha hiyo aliahidiwa dau nono la milioni hamisini
endapo atafanikisha kukamatwa kwa Eddy tu.
Raisi
Godwin akiwa ameongozana na walinzi wake pamoja na mwaye kipenzi Manka,
wakafika uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya kuelekea nchini
Marekani, Miami kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka. Manka katika
kutazama tazama kwake, akamuona mwanaume mmoja mwenye sura ya kuvutia
kiasi kilicho mfanya kusimama kwa muda akiwa ameduwaa.
“Vipi mbona unashangaa?”
Raisi Praygod alimuuliza Manka baada ya kusimama kabisa akimshangaa mawanaume huyo.
“Hapana baba hakuna kitu”
“Una uhakika?”
“Ndio baba”
Manka
alizungumza huku akiendelea na safari, wakati huu mzee Godwin akamshika
mkono kabisa, kitendo kilicho mnyima uhuru Manka cha kumtazama mwanaume
ambaye ametoke kumtamani kwa dakika chache alizo weza kumuona.
***
Baada
ya ndege kutua katika kiwacha cha mwalimu J.K Nyerere, abiria wote
wakashuka kwenye ndege akiwemo Eddy na wezake. Sheria waliyo iweka
tangu wakiwa wapo nchini Misri, ni kwamba wakishuka kwenye ndege,
wasijifanye kama wana juana, ila Sa Yoo ataongozana na Shamsa. Ila Eddy
atakuwa peke yake, huku Phidaya naye akiwa peke yake. Madam Mery naye
akiwa peke yake, Rahab akiwa peke yake huku raisi Praygod akiwa peke
yake ila nyuma ya Eddy.
Macho ya Eddy yakaweza kuona msafara mzima wa raisi Praygod unavyo
ingia katika sehemu ya abiria wanao safari. Macho ya Eddy yakagongana na
macho ya Manka ambaye anamtambua vizuri, akaona jinsi Manka anavyo
mshangaa kiasi cha kuhisi amegundulika.
Kitendo
cha raisi Praygod kusimama na kuzungumza na Manka, kikaanza kupandisha
hasira ya Eddy, akataka kuruka katika vizuizi vilivyopo katika upande
wake na kuelekea upande wa mzee Godwin anaye lindwa na askari wengi, ila
kwa haraka raisi Praygod aliye valia kofia kubwa la kizee akamuwahi na
kumshika mkono kwa nyuma Eddy.
“Hapa sio eneo lake Eddy utasababisha mpango kuharibika”
0 comments:
Chapisha Maoni