Akielezea
tukio hilo jana (Alhamisi Julai 6) , Mkuu wa Operesheni Maalumu za
Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas alisema
tukio hilo lilitokea Jumatano saa nne usiku katika msitu wa
Ngomboroni Kata ya Ikwiriri, Wilaya ya Ikwiriri.
Wahalifu
hao waliuawa na askari wa operesheni maalumu wakiwa katika doria za
ufuatiliaji wahalifu sugu wanaojihusisha na mauaji yanayoendelea katika
kanda hiyo ya kipolisi.
Alisema
askari wakiwa na mtuhumiwa mmoja muhimu anayeshiriki katika mauaji
hayo ambaye alikamatwa, alikubali kwenda kuwaonyesha polisi mahali
ambapo ni maficho ya wenzake.
“Baada
ya kufika eneo la msitu wa Ngomboroni kikundi cha watu wanaokadiriwa
kufikia watano walikurupuka kutoka kwenye kichaka na kuanza kukimbia
ndipo polisi kwa tahadhari kubwa walianzisha mashambulizi na kufanikiwa
kumjeruhi mhalifu mmoja kwa risasi, katika mashambulizi hayo mtuhumiwa
aliyekuwa mkononi mwa polisi naye alijaribu kutoroka na hivyo
kupelekea kumjeruhi kwa risasi hivyo idadi yao kufikia wawili,” alisema.
Aliongeza;
“majeruhi hao wawili walifariki dunia njiani wakati wakipelekwa
hospitali kwa matibabu kutokana na kuvuja damu nyingi iliyosababishwa
na majeraha ya risasi waliyoyapata. Miili ya marehemu imehifadhiwa
katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.”
Kamishna
Sabas alisema katika tukio hilo wamefanikiwa kupokonya silaha mbili
aina ya SMG na Shotgun moja pamoja na risasi tisa.
Kamishina
Sabas amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa
wahalifu wengine waliosalia na kwamba zawadi nono bado ipo pale pale
na itatolewa kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa sahihi kuhusiana na
wahalifu wanaojihusisha na mauaji katika kanda maalumu ya Rufiji.
0 comments:
Chapisha Maoni