test

Ijumaa, 7 Julai 2017

Bradley Lowery: Shabiki Mtoto wa Sunderland afariki Dunia



Baada ya kuugua kwa muda mrefu, Bradley Lowery (6) amefariki dunia leo. Lowery anatambulika kwa kuwa mshabiki mkubwa wa Sunderland ya nchini Uingereza na alipata umaarufu mkubwa Duniani baada ya kugundulika na maradhi ya neuroblastoma aina adimu ya kansa duniani.
Bradley aligundulika na maradhi hayo akiwa na umri wa miezi 18 na alikuwa rafiki wa karibu wa mshambuliaji wa klabu hiyo ya Sunderland Jermain Defoe.

Kifo chake kimethibitishwa na wazazi wake kupitia ukurasa maalum wa harakati za Bradley Lowery.
“Kijana wangu ameondoka na malaika leo tarehe 07/07/17 saa 7 na dakika 35 katika mikono ya mama na baba huku akiwa amezungukwa na familia yake” ilisomeka sehemu ya ujumbe huo ambao nimekuekea hapo chini

Hapa chini nimekuekea video fupi iliyoandaliwa na BBC na kurushwa kupitia mtandao wa Twitter


Chini hapa nimekuekea picha tano za matukio tofauti tofauti enzi za uhai wake

Bradley Lowery akiwa na mama yake Gemma Lowery


Bradley Lowery alipokua mmoja wa wasindikizaji wa timu ya Taifa ya England ilpocheza na Lithuania mwezi march mwaka huu


Bradley Lowery kwenye Red Carpet ya BBC katika shindano la personality of the year


Bradley na baba yake Carl katika mechi kati ya Everton na Sunderland


Bradley na rafiki yake kipenzi Jermain Defoe hospitalini

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni