Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
ameridhia maombi ya kustaafu mapema kwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Mhe. Prof. John Eudes Ruhangisa.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa
Mhe. Rais Magufuli ameridhia maombi ya kustaafu mapema kwa Prof. John
Eudes Ruhangisa kuanzia 06 Julai, 2017.
Mhe. Prof. John Eudes Ruhangisa alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
0 comments:
Chapisha Maoni