Bodi
ya Wadhamini iliyo chini ya Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi
ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, imeiomba
Mahakama Kuu iitendee haki kwa kuithibitisha kama bodi halali ya chama
hicho, ili iweze kufuta kesi zilizofunguliwa dhidi ya Lipumba na
wenzake, kwa madai zilifunguliwa na Bodi isiyo halali.
Wakati
akizungumza na waandishi wa habari, jana Julai 6, 2017 katika Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Slaam , Katibu wa Bodi hiyo, Thomas Malima alidai
kuwa mahakama hiyo haikuwatendea haki kwa kutothibitisha uhalali wa bodi
hiyo pamoja na kutowatambua mawakili wake.
“Mahakama
haikutupa haki ya kutusilikiliza na kuithibitisha bodi yetu ambayo ni
halali, mawakili wanaojiita wa bodi ya CUF ndiyo wale tuliowafukuza
kazi, ambao kwa sasa ni sawa na mawakili wa mahakama na si wa chama
chetu hatuwatambui, sisi ndio wenye mamlaka ya kufuta kesi,” alisema Malima.
Aidha,
Bodi ya Wadhamini iliyo chini ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif
Shariff Hamad imefungua mashauri takribani sita dhidi ya Lipumba na
wenzake ikiwemo shauri la kuzuia utolewaji wa fedha za rudhuku ya chama
hicho kwa Lipumba.
Na
kwamba Bodi ya Lipumba inadai kuwa kesi hizo zimefunguliwa kinyume na
sheria kwa kuwa yenyewe ndiyo yenye uhalali wa kufungua kesi za chama
hicho.
0 comments:
Chapisha Maoni