Chama
cha Alliance For Democratic Change (ADC) wameitaka Chadema itoe msimamo
wake kuhusu kauli ya mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu kutaka
jumuiya za kimataifa zisitishe misaada kwa Tanzania.
Katibu Mkuu wa ADC, Doyo Hassan amesema kama huo hautakuwa msimamo wa Chadema ,Lissu anapaswa kuomba radhi.
Amesema kauli ya kutaka misaada isitishwe hailengi kuwatakia mema Watanzania.
"Tunadhani matatizo yetu ya ndani ni vema tukapambana nayo kuliko kutangazia ugomvi wako kwa mtu asiyekuhusu.’’
"Kwa
kauli hii hizi za Chadema ni wazi wameshindwa mapambano ya ndani na
sasa wanafikiria njia nyingine ambazo ni hatari zaidi katika nchi yetu,"amesema Hassan.
Amesema
kama Chadema imeshindwa kupambana na CCM na Serikali yake ni wazi
wawaeleze wafuasi wao kuliko kutoa matamshi ambayo yanahatarisha ustawi
wa taifa letu.
0 comments:
Chapisha Maoni