Mbunge
wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amekuja juu na kutoa ya moyoni akionekana
kutofurahishwa na taarifa iliyosambaa kwenye vyombo mbalimbali vya
habari ikiwemo mitandaoni ikitokea Chama cha demokrasia na maendeleo-
CHADEMA.
Kauli za Zitto zilifuatia taarifa aliyoiona kwenye ukurasa wa Twitter iliyosema; “CHADEMA waitaka Jumuiya ya kimataifa kuinyima misaada Tanzania kutokana na ukiukwaji wa Demokrasia mfano, kukamatwa kwa viongozi wa upinzani”
Baada ya kuiona hiyo taarifa Zitto Kabwe aliandika “Huu
ni uhayawani, hii ni nchi huru, kukaribisha wageni kuingilia mambo yetu
ni upuuzi na umazwazwa, tupambane ndani kuleta demokrasia .NDANI”
Baada
ya Zitto kuonyesha dhahiri msimamo wake, baadhi ya Followers wake
kwenye Twitter walimuandikia kila mmoja na maoni yake na yeye akawajibu
kama inavyoonekana hapa chini.
0 comments:
Chapisha Maoni