Mbunge
wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amesema suala la mauaji
yanayoendelea katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji, linahitaji
mshikamano na kuwa mauaji hayo hayapewi nafasi ya kuendelea.
Zitto
ameandika hayo leo (Jumatano) kwenye ukurasa wake wa facebook na
twitter na kutaka taifa lizungumze lugha moja ili kukabiliana na mauaji
hayo.
“Ninarejea
wito nilioutoa siku zilizopita kuwa ninatarajia Kamati ya Bunge ya
Ulinzi na Usalama itakwenda eneo la MKIRU kuzungumza na wananchi wa kule
ili kupata maarifa ya mbinu za kuishauri na kuisimamia Serikali
kudhibiti mambo na kuimarisha usalama.” Ameandika Zitto.
0 comments:
Chapisha Maoni