Viongozi
wawili wa serikali za mtaa katika Kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti
mkoani Pwani wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa
kuamkia leo Jumatano, Juni 28.
Kwa
mujibu wa taarifa ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Pwani, Onesmo Lyanga zimeeleza kuwa waliouawa ni Mtendaji wa Kijiji cha
Mangwi, Shamte Makawa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko
Nicholaus.
Aidha, kamanda wa polisi amesema kuwa tayari askari wamekwenda eneo hilo kwa ajili ya hatua zaidi.
Hadi
sasa watu zaidi ya 37 tayari wameuawa katika mfululizo wa matukio
ambayo bado Polisi hawajafahamu ni nani mhusika na lengo haswa la
kufanya hivyo.
0 comments:
Chapisha Maoni