Waziri
wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mkoani
Singida, Mwigulu Nchemba leo bungeni amefunguka na kuomba radhi dhidi ya
vitendo vya jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa kupambana na watu wenye
ulemavu.
Mwigulu
Nchemba amekiri kuwa jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa mno kwa watu
hao na kusema serikali wamepokea jambo hilo na kuahidi kulifanyia kazi
ili siku nyingine lisijirudie.
"Kwanza
naomba niombe radhi kwa jambo hili na naomba salamu zangu ziwafikie
watu wenye ulemavu, ni kweli kwamba kwa kuzingatia hali yao jeshi la
polisi lilitumia nguvu kubwa, ila sisi kama serikali tumeshawasiliana na
TAMISEMI na kuzungumza nao juu ya mambo yao, lakini pia tumepokea jambo
hili na tunalifanyia kazi ili siku nyingine jambo hili lisijirudie" alisema Mwigulu Nchemba
Mnamo
tarehe 16, Juni, 2017 jijini Dar es Salaam jeshi la polisi lilitumia
nguvu kubwa ikiwepo kuwapiga na kuwadhalilisha watu wenye ulemavu ambao
walikuwa wamejikusanya katika barabara ya Sokoine, Posta Jijini Dar es
salaam ili kwenda kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, kuwasilisha
malalamiko dhidi ya askari wa usalama wa barabarani kuwakamata na
kuwazuia kuingia katika jiji. Lakini pia walikuwa wakipigania haki yao
ya kuwa na maeneo ya kuegesha vifaa vyao katikati ya jiji.
0 comments:
Chapisha Maoni