Wananchi
wa vijiji vya Bulangwa na Katente mkoani Geita,wameliomba Bunge la
Tanzania kufanya marekebisho ya muda wa ukomo wa urais kutoka miaka kumi
ya sasa hadi miaka ishirini ili kumuwezesha Rais Dk.John Pombe Magufuli
kuendelea kubakia madarakani.
Wananchi
hao walitoa ushauri huo jana katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na
mbunge wa jimbo la bukombe mh. Dotto biteko kwa ajili ya kumpongeza Rais
Dk.John Pombe Magufuli kwa namna alivyosimamia sekta ya madini,mkutano
ambao ulihudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh.Costantine
Kanyasu.
Akiwahutubia
wananchi,Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati
ya Nishati na Madini Mh. Dotto Biteko,alisema kazi ya kupigania
rasilimali za taifa inayofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli si ya
lelemama,huku Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh. Kanyasu akisema
serikali ya awamu ya tano haiwachukii wawekezaji, bali inawachukia
waporaji wa raslimali za nchi.
Ripoti
ya kamati ya pili ya mchanga wa madini wa Makinikia,iliyowasilishwa
Juni 12 mwaka huu kwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kamati hiyo
Prof.Nehemiah Ossoro ilibaini taifa kupoteza shilingi Trilioni 252
kupitia usafirishaji wa mchanga wa madini ya makinikia nje ya nchi
kuanzia mwaka 1998 hadi kufikia mwaka huu,huku ikiwahusisha baadhi ya
mawaziri wa zamani wa nishati na madini waliohusika kuingia mikataba
mibovu iliyoisababishia serikali hasara.
0 comments:
Chapisha Maoni