Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Prof: Makame Mbarawa (katikati)
akishuhudia makabidhiano ya mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha
Bandari kati ya Serikali na Kampuni ya China Harbour Engineering. Kulia
ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA). Mhandisi
Deusdedit Kakoko na kushoto ni Mtedaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. XU
XINPEI. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).Benjamin Sawe-Maelezo
Mamlaka
ya Bandari nchini (TPA), imesaini mkataba wa upanuzi na uongezaji wa
kina cha bandari utakaowezesha bandari ya Dar es Salaam kupokea meli
kubwa za mizigo na kushindana na bandari nyingine katika pwani ya bahari
ya hindi.Upanuzi
huo utakaofanywa na kampuni ya China Harbor Construction ya China
utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 336 na utadumu kwa miezi 36,
ambapo utahusisha uongezaji wa kina cha lango la bandari na uongezaji wa
kina cha maji kati ya gati namba 0, 1 hadi 7.
Akizungumza
katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hatua hiyo inalenga kuifufua
upya bandari ya Dar es Salaam ili ifanye kazi kwa ushindani na kuhudumia
wateja wengi kuliko ilivyo sasa.
“
Kukamilika kwa upanuzi na uongezaji wa kina cha maji katika gati namba 1
hadi 7 kutoka mita 8 hadi 15 kutawezesha meli kubwa na za kisasa zenye
uwezo wa kubeba hadi makontena elfu kumi na tisa kutia nanga katika
bandari ya Dar es Salaam na kuongeza ufanisi na kukuza uchumi wa
Tanzania”, amesema Prof. Mbarawa.Aidha
Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa pamoja na upanuzi wa bandari ya Dar es
Salaam Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu wezeshi ya reli na
barabara ili kuhakikisha mizigo haikai muda mrefu bandarini.“Ujenzi
wa reli ya kisasa ya Standard Gauge toka Dare s Salaam hadi Kanda ya
Ziwa na Kigoma na ufufuaji wa reli ya Tazara kutawezesha bandari ya Dar e
s Salaam kufanya kazi kwa ufanisi na kuvutia wafanyabiashara wengi
hivyo nawataka wafanyakazi wote wa bandari kufanyakazi kwa bidii na
uadilifu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko amesema kiasi cha dola za
Marekani milioni 421, kitapatikana kwaajili ya ujenzi huo ambapo kati ya
fedha hizo Benki ya Dunia itatoa mkopo wa masharti nafuu wa dola
milioni 345.
Kukamilika
kwa ujenzi huo kutaondoa adha ya baadhi ya meli kusubiri kwa muda mrefu
kupata nafasi ya kutia nanga na kutaongeza hadhi ya bandari ya Dar es
salaam na kuvutia wasafirishaji wengi kutoka ndani na nje ya nchi.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA). Mhandisi Deusdedit
Kakoko kulia na Mtedaji Mkuu wa Kampuni ya China Harbour Engineering Bw.
XU XINPEI wakionyesha mkataba wa makubaliano ya upanuzi na uongezaji wa
kina cha Bandari kwa wadau wa sekta ya usafirishaji baada zoezi la
utiaji saini wa mkataba huo kukamilika. (Picha na Benjamin Sawe-
Maelezo).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Prof: Makame Mbarawa akiongea na wadau wa sekta ya usafirishaji kabla ya zoezi la utiaji saini wa mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha Bandari kati ya Serikali na Kampuni ya China Harbour Engineering. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko na kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Bw. Mkinga Mkinga. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Prof: Makame Mbarawa akiongea na wadau wa sekta ya usafirishaji kabla ya zoezi la utiaji saini wa mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha Bandari kati ya Serikali na Kampuni ya China Harbour Engineering. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko na kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Bw. Mkinga Mkinga. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).
0 comments:
Chapisha Maoni