Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Felix Ngamlagosi kuanzia
leo tarehe 11 Juni, 2017.
Maamuzi
haya yamekuja siku mbili baada ya habari za kampuni ya IPTL kutaka
kuongezewa mkataba wa uzalishaji umeme ambapo pia Kituo cha sheria na
haki za Binadamu kilijitokeza na kusema hakikubaliani na mkataba huo
kuongezwa kwani kampuni hiyo inahusishwa na kashfa ya uchotwaji wa
Mabilioni kupitia account ya ESCROW.
Hata hivyo baada ya kituo hicho cha LHRC kujitokeza kuongea, EWURA walijitokeza na kusema "Kuna
vitu viwili vya kuzingatia hapa, EWURA tunachodili nacho sasa hivi ni
leseni ya IPTL ambayo aliipata 1996 ikiwa ni ya miaka 21 na inaisha July
2017"
“Sheria
iliyoanzisha EWURA na sheria ya UMEME zinataka mtu yeyote anavyoomba
leseni EWURA itoe taarifa kwa umma ili watu watoe maoni au pingamizi,
hicho ndicho tulichokifanya na hatuendi kwa siri…. tumetoa siku 21 za
kupokea maoni, kinachotendeka hapa ni IPTL kutaka kuomba kuongeza
leseni"
0 comments:
Chapisha Maoni