Aliyekuwa
Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa ametakiwa kuripoti katika Ofisi
ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) leo saa nne
asubuhi.
Lowassa
ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) amepewa wito huo kwa njia ya barau bila kuelezwa sababu za
yeye kutakiwa kufanya hivyo.
Msemaji
wa CHADEMA, Tumaini Makene na Lowassa mwenyewe wote wamethibitisha
kupata taarifa za wito huo huku wakisema si chama wala mhusika anayejua
sababu za kuitwa.
Aidha,
katika mahojiano aliyofanya Lowassa na The Citizen kwa njia ya simu,
amesema kuwa anadhani kuitwa kwake kuna uhusiano na kauli aliyoitoa
mwishoni wa juma wakati wa futari kuhusu Masheikh wa Uamsho.
Lowassa
alimtaka Rais Magufuli kuingilia kati suala hilo ambapo Masheikh kadhaa
wanashikiliwa kwa zaidi ya miaka minne sasa bila maendeleo yoyote ya
tuhuma zinazowakabili. Masheikh hao ambao walikamatwa Zanzibar
wanatuhumiwa kwa ugaidi ambapo Lowassa alitaka Rais aingilie kati ili
kesi hiyo iweze kusikilizwa.
“Sina
hakika kama hii ndio sababu, lakini nahisi tu. Ila ukweli utafahamika
nitakapokutana na DCI,” alisema Lowassa kwenye mahojiano hayo ya simu.
0 comments:
Chapisha Maoni