Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Waziri
Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa amepata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa
Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo
Jumanne, saa 4 asubuhi kwa ajili ya mahojiano.
Mhe.
Lowassa ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA) kupitia CHADEMA, kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, hajapewa
maelezo wala ufafanuzi wowote kuwa mahojiano hayo yatahusu nini hasa.
Tayari
Chama kimetoa maelekezo kwa Kurugenzi ya Katiba na Sheria ya Chama
kuhakikisha kuwa Mhe. Lowassa anapata msaada wa kisheria wakati wa
mahojiano hayo.
Taarifa
za awali zinaonesha kuwa mahojiano hayo yanahusishwa na kauli za Mhe.
Lowassa alizotoa katika nyakati tofauti hivi karibuni wakati akishiriki
futari pamoja na Watanzania wenzetu Waislam waliokuwa katika Mwezi
Mtukufu wa Ramadhan, ambapo amekuwa kiitaka Serikali kuzingatia misingi
ya utawala bora kama mojawapo ya misingi muhimu ya kuendesha nchi kwa
ajili ya ustawi na maendeleo ya Watanzania wote.
Imetolewa Jumatatu, Juni 26, 2017 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
0 comments:
Chapisha Maoni