“Nimpongeze sana Mhe Rais John Pombe
Magufuli kwa uamuzi na hatua ambazo amechukua kuhusu jambo hili, na hasa
pale anapowashirikisha wananchi, ni jambo muhimu sana.
Maneno hayo yalisema jana na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward
Lowassa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la
mchanga wa madini (makinikia) ambalo limeonyesha kuwa Tanzania impoteza
zaidi ya trilioni 100 tangu mwaka 1998 hadi Machi mwaka 2017.
Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alisema
anampongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza maamuzi ambayo ni ya UKAWA
kwani kipindi anazunguka kuomba kura kwa wananchi alipopita maeneo yenye
madini aliyazungumza haya yanayotekelezwa leo.
“Nampongeza kwa kutekeleza yale maamuzi ambayo ni ya UKAWA. Nilipokuwa
kwenye kampeni ya kuomba kura, hata pale Geita, nilieleza jambo hilo,
nikasema hivyo hivyo alivyosema yeye kwamba nikiingia madarakani
nitaunda tume ya kuchunguza jambo hili ili mtanzania awe ndiye anapata
sehemu kubwa ya faida kuliko mgeni.”
Aidha, Lowassa amesema kuwa, ni kweli mikataba ya madini ina matatizo na
hata yeye alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu aliwaita wawekezaji hao wakakaa
na na kuzungumza, lakini jambo gumu lilikuwa ni kamba, mikataba
ukishaiweka saini inakuwa migumu sana kubadilisha.
Lowassa alieleza kwamba baada ya kuongea nao kwa muda walikubali na kuongeza kidogo mirahaba lakini haikutosha.
“Matumaini yangu ‘figure’ (namba) hizo ni za kweli, kama ni za kweli,
tumeliwa kweli kweli,” alisema Lowassa alipokuwa akizungumzia mahesabu
yaliyowasilishwa katika ripoti za uchunguzi kuhusu kiasi cha fedha
ambazo Tanzania imepoteza.
0 comments:
Chapisha Maoni